UKURASA WA 846; Usifanye Vitu Hivi…

By | April 25, 2017

Rasilimali moja ambayo ina ukomo mkubwa na muhimu sana kwenye mafanikio ni muda. Muda ni muhimu, lakini pia muda ni mchache, masaa 24 kwa siku, hakuna nyongeza, hata ufanye nini.

IMG-20170321-WA0000

Lakini katika muda huu, wapo wanaofanikiwa, na wapo wanaoshindwa kufanikiwa. Wapo wanaoweza kufanya yale muhimu kwao na wapo ambao muda hauwatoshi kabisa.

Kinachowafanya wengi muda usiwatoshe, ni kutaka kufanya kila kitu wao peke yao. Wanakuwa na imani kwamba wao pekee ndiyo wanaoweza kufanya vizuri, wengine hawawezi. Na hata wakiwapa wengine wafanye, basi lazima wawafuatilie kwa karibu.

SOMA; Usifanye Kabisa Biashara Hii, Ni Kupoteza Muda Wako…

Vipo vitu ambavyo vinastahili ufuatiliaji huo wa karibu, lakini vitu vingi unavyong’ang’ania kufanya kwenye maisha yako, wapo watu ambao wangeweza kuvifanya vizuri tu. Kama ungekuwa tayari na kuwapa wengine wavifanye, wewe ungekuwa na muda zaidi wa kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwenye maisha yako na mafanikio yako.

Hivyo ninachotaka kukuambia leo rafiki, usifanye kitu chochote ambacho mtu mwingine anaweza kukifanya. Kila unachofanya kila siku, jiulize, je hichi ni mimi tu ndiyo naweza kufanya? Kama jibu ni ndiyo basi fanya, kama yupo mwingine anayeweza kufanya, mpe yeye afanye, ili wewe uweze kupata muda zaidi.

Kwa dunia ya sasa siyo tu mtu anaweza kufanya, bali pia zipo programu zinazoweza kufanya mambo mengi ambayo unakazana kufanya mwenyewe. Programu hizi zinakurahisishia kazi na kukuokolea muda. Hivyo uliza pia kama kuna programu inayoweza kukusaidia kufanya kile unachotaka kufanya.

Ulinde muda wako kwa kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwako, mengine angalia namna yanavyoweza kufanyika na wengine au kufanywa na programu zinazoweza kuyafanya vizuri.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.