UKURASA WA 877; Dunia Inaendeshwa Kwa Hisia…

By | May 26, 2017

Japokuwa tafiti nyingi zinafanywa na data kupatikana kujua vitu gani vinawafanya watu kuchukua maamuzi fulani, labda kununua au kukubali kitu fulani, kipo kitu kimoja ambacho kinaongoza maamuzi ya watu wengi duniani. Kitu hicho ni hisia. Hisia zinaendesha dunia, na ndiyo maana utaona vitu kama mapenzi, chuki na wivu vinatawala maamuzi ya wengi.

Watu wanafanya kitu ambacho wanakipenda, ambacho wanajisikia vizuri kufanya. Hivyo unapotaka watu wafanye kitu, unapotaka kuwashawishi watu wafanye kile unachowataka wafanye, hakikisha unawapa kile kitu wanachopenda. Hakikisha unawafanya wajisikie vizuri kwa kufanya kitu hicho, kama ni kununua basi wajisikie vizuri wakinunua kile unachowauzia.

Watu wanaepuka vile wanavyovichukia, wanahakikisha maamuzi yao ni dhidi ya kile wanachochukia, hivyo unahitaji kuepuka yale ambayo watu wanayachukia kama unataka kupata watu wengi wa kukubaliana na wewe na kufanya kile unachowashawishi wafanye.

Badala ya kutumia nguvu nyingi kuwashawishi watu wachukue hatua fulani, kwa kuwapa ukweli na data zinazodhibitisha, wape sababu nzuri itakayoshika hisia zao kwa nini wafanye kile unawataka wafanye.

SOMA; Kwa Nini Hisia Bado Zinatushinda Kudhibiti Na Namna Ya Kuzidhibiti.

Na ipo njia moja ya uhakika ya kuhakikisha unawapa watu kile wanataka kwa hisia zao, kuwapa watu busara ya hali ya juu. Kwa busara hiyo, watu hawatahangaika kujua kingine zaidi ya kile unawapa. Ndiyo maana ni muhimu sana chochote unachofanya, uwe unakujua vizuri na kwa undani zaidi. Hii itakusaidia kuweza kuwaeleza watu kwa namna kinavyowasaidia na kuwawezesha kuchukua hatua.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.