UKURASA WA 945; Ongoza Mabadiliko…

By | August 2, 2017

Watu wanaofanikiwa ni wale ambao wapo tayari kubadilika, lakini watu wanaofanikiwa zaidi ni wale ambao wanaongoza mabadiliko. Sijui kama umeiona tofauti hapo, lakini wacha twende taratibu.

Kuwa tayari kubadilika ni pale unapoona mabadiliko yako mbele yako na kuyafanyia kazi badala ya kuyakwepa au kuyapuuza. Unaona wengine wanabadilika hivyo na wewe inabidi ubadilike, ili usiachwe nyuma. Na hapo kweli unanufaika kama ambavyo wengine wanaobadilika wananufaika.

Kuongoza mabadiliko ni pale ambapo wewe unaanzisha mabadiliko, kwa kujaribu vitu ambavyo havijafanywa kabisa na wengine, kuanza kuvifanya na kupata njia bora zaidi, ambapo wengine wanalazimika kubadilika kwa kukuona wewe ukibadilika. Hapa unanufaika zaidi kwa sababu unakuwa mbele ya kundi. Unanufaika zaidi kwa sababu mpaka wengine wabadilike na kukufikia wewe, unakuwa umeshapiga hatua kubwa zaidi.

SOMA;  Wakati Sahihi Wa Kufanya Mabadiliko Ni Huu…

Hivyo popote ulipo, usisubiri tu mabadiliko ya nje ndiyo uyafuate, badala yake tengeneza mabadiliko yako wewe mwenyewe. Ukiweza kutumia akili yako vizuri, utaziona fursa nyingi za mabadiliko ambazo unaweza kuzifanyia kazi.

Kuongoza mabadiliko unahitaji kuwa mdadisi, uhoji, ufanye utafiti, uwe mbunifu na pia uwe na uthubutu wa kufanya mambo mapya. Upo uwezekano mkubwa wa kushindwa kwenye mengi utakayojaribu, lakini pia utaweza kufanikiwa kwenye machache kati ya hayo.

Ongoza mabadiliko na utaongoza mafanikio yako wewe mwenyewe.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.