Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA ASUBUHI; UNAHITAJI NYAKATI NGUMU…

By | July 11, 2020

“There should be a science of discontent. People need hard times and oppression to develop psychic muscles.” — Frank Herbert Moja ya nadharia za mageuzi inasema kiungo cha mwili kinachotumika sana huwa kinakuwa imara huku kile kisichotumika kikiwa dhaifu na hata kupotea kabisa. Na njia rahisi ya kupima hilo ni (more…)

2018; Watu Wenye Hofu…

By | July 10, 2020

Watu wenye hofu huwa wanapenda kuzungukwa na watu wenye hofu. Ungeweza kufikiri kwamba watu hao wangependa kuzungukwa na wasio na hofu, wanaojiamini ili nao washinde hofu zao. Lakini hivyo sivyo ilivyo, watu wenye hofu wanapenda kuzungukwa na wengine wenye hofu ili kuhalalisha hofu zao. Wanachotaka kuamini ni kwamba hofu walizonazo (more…)

2017; Urahisi Na Raha Ya Kufanya…

By | July 9, 2020

Kanuni muhimu kabisa ya uchumi ni hii, kadiri kitu kinavyopatikana kwa wingi na urahisi, ndivyo thamani yake inakuwa ndogo na watu kutokuwa tayari kulipa gharama kubwa kukipata. Hii ndiyo kanuni unayopaswa kuendesha nayo maisha yako, kupima kila unachotaka kufanya ili kujua thamani yake. Kama unachofanya kinafanywa na kila mtu, usitegemee (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; SIYO WINGI WA TAARIFA, BALI UNAZITUMIAJE…

By | July 9, 2020

“We live in the age of philosophy, science, and intellect. Huge libraries are open for everyone. Everywhere we have schools, colleges, and universities which give us the wisdom of the people from many previous millennia. And what then? Have we become wiser for all this? Do we better understand our (more…)

2016; Kelele Na Kazi Haviendi Pamoja…

By | July 8, 2020

Upo usemi baina ya wawekezaji kwamba ukiona mkurugenzi mkuu (CEO) wa kampuni anaongea sana kwenye vyombo vya habari, basi jua kuna tatizo kwenye kampuni hiyo. Kuna kitu hakipo sawa au mkurugenzi huyo hafanyi kazi yake vizuri. Usemi huo una ukweli ambao ukiujua na kuutumia utakusaidia. Ni kweli kwamba kelele na (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; SIYO KUWASHINDA WAO, BALI KUJISHINDA MWENYEWE…

By | July 8, 2020

“Pay bad people with your goodness; fight their hatred with your kindness. Even if you do not achieve victory over other people, you will conquer yourself.” — HENRI AMIEL Unapolipa ubaya kwa wema, Unapolipa chuki kwa upendo, Lengo siyo kuwashinda wale wanaokufanyia hayo, Bali lengo ni kujishinda wewe mwenyewe. Mpumbavu (more…)

2015; Saa Moja Ya Kufanya Kazi…

By | July 7, 2020

Kama ambavyo mwanafalsafa Seneca amewahi kuandika, tatizo la muda siyo kwamba ni wa uhaba na hautoshi, bali ni mwingi na tunautawanya hovyo. Ndiyo maana swali maarufu la kujiuliza kama leo ingekuwa siku yako ya mwisho hapa duniani ungefanya nini, linatusaidia sana kuweka vipaumbele vyetu sawa. Tunapojua kwamba bado tuna muda, (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; KAZI BORA ZINAFANYIKA KWENYE UTULIVU…

By | July 7, 2020

“Without great solitude, no serious work is possible.” — Pablo Picasso Bila ya utulivu, huwezi kufanya kazi ambayo ni bora. Bila ya kuondokana na kelele na usumbufu mwingine wa akili yako, haiwezi kutulia na kuja na mawazo bora. Wanasayansi, wanafalsafa, waandishi, wajasiriamali na watu wengine, huwa wanapata mawazo bora pale (more…)