Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA ASUBUHI; KITU MUHIMU ZAIDI KWAKO KIFANYA…

By | July 1, 2020

“Concentrate on what’s in front of you like a Roman. Do it like it’s the last and most important thing in your life.” – Marcus Aurelius Wengi huanza siku zao wakiwa na mipango mbalimbali, Wanamaliza siku hizo wakiwa wamechoka kweli kweli, Lakini wakiangalia walichofanya, hawaoni. Wamesumbuka siku nzima na kuchoka, (more…)

2008; Dalili Ya Hofu Isiyoonekana Wazi Wazi…

By | June 30, 2020

Kila mtu huwa ana dalili fulani za hofu, pale anapokuwa na hofu, mwili wake huwa unamsukuma kufanya kitu fulani, hata kama hajui. Kuna ambao hung’ata kucha, kuna ambao mikono hutetemeka na wengine kutokwa jasho, hata kama hakuna joto. Ipo dalili ya kiakili ya hofu, ambayo huwa inawapata walio wengi, lakini (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; FANYA AU USIFANYE, USIWEKE SABABU…

By | June 30, 2020

“People who want to write either do it or they don’t.” — Octavia Butler Kama kuna kitu unataka kufanya, una machaguo mawili, kukifanya au kutokukifanya. Chochote zaidi ya hayo mawili ni kujidanganya tu. Kama unataka kuandika, unachagua kuandika au kutokuandika, Kujiambia utaandika ukiwa na muda ni kujidanganya. Kama unataka kuanzisha (more…)

2007; Fursa Iliyokuwa Inakusubiri Wewe…

By | June 29, 2020

Ukiona watu wanakuna kwako na fursa, wanakuonesha fursa inayokufaa sana na kukushawishi ujiunge na fursa hiyo la sivyo utaikosa basi kuwa na uhakika kwenye jambo hili, wewe ni fursa kwa watu hao. Kama wanachokuambia ni fursa kweli, unafikiri ingekaa muda wote ikusubiri wewe? Unafikiri hao wanaokusisitiza ni fursa wangepoteza muda (more…)

2006; Uhuru Ni Kujitambua…

By | June 28, 2020

Mtoto mdogo akitaka kitu anakitaka kama anavyotaka yeye, hawezi kukubali kitu kingine isipokuwa kile anachotaka yeye. Kupata kile anachotaka anaweza kufikiri ni uhuru, lakini huo siyo uhuru. Uhuru siyo kupata kile ambacho mtu anataka kwa namna anayotaka yeye. Huko ni kuendeshwa na hisia au mihemko na siyo kuwa huru. Uhuru (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; WATAKUHUKUMU KWA UNACHOFANYA…

By | June 28, 2020

“People who watch you judge you on what you do, not how you feel.” – CUS D’AMATO Watu wanaokuangalia huwa wanakuhukumu kwa kile unachofanya na siyo jinsi unavyojisikia. Unachofanya kinaonekana na kila mtu, Hisia zako unazijua mwenyewe. Hivyo unapaswa kuwa makini, usiruhusu hisia zikusukume kufanya kile ambacho siyo sahihi. Hata (more…)

2005; Motisha Ni Nyenzo Kwa Watu…

By | June 27, 2020

Mwanahisabati Pythagoras aliwahi kusema nipe nyenzo ndefu na mahali pa kusimama na nitaweza kuisogeza dunia. Hapa alionesha jinsi ambavyo nyenzo ina nguvu ya kufanya makubwa, yale ambayo kwa hali ya kawaida hayawezekani. Chukua mfano wa nyenzo kwenye maisha yetu ya kila siku, kung’oa msumari mahali kwa mikono yako ni zoezi (more…)

2004; Dakika Kumi Zinaweza Kufanya Nini?

By | June 26, 2020

Kitu kimoja ninachokiamini, na nitaendelea kuamini hivyo maisha yangu yote ni kwamba wale wanaosema hawana muda wa kufanya vitu fulani wanavyotaka kufanya huwa wanadanganya. Siyo kweli kwamba hawana muda, ila tu hawataki kufanya, sasa kwa kuwa hawataki kuukabili ukweli, wanatumia kisingizio cha muda. Kwenye siku kuna masaa 24 ambayo ukiyageuza (more…)