Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; KUNA WAKATI KUISHI NI TENDO LA KISHUJAA…

By | February 4, 2018

Sometimes even to live is an act of courage. – Lucius Annaeus Seneca Hongera rafiki kwa siku hii nzuri na ya kipekee wana kwetu. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA. Pia kwa mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tutaweza kufanya (more…)

UKURASA WA 1130; Njia Mbili Za Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo…

By | February 3, 2018

Kuna mambo ambayo tunakuwa tumepanga au kupangiwa kufanya, lakini kutokana na changamoto mbalimbali, tunashindwa kuyafanya. Haya hutuletea msongo wa mawazo na kutuzuia hata kufanya mambo mengine kwa utulivu na amani ya moyo. Watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanya makubwa kutokana na msongo walionao kwa yale waliyoshindwa kufanya au waliyofanya na wakashindwa. (more…)

UKURASA WA 1128; Kuepuka Kukosolewa…

By | February 1, 2018

Meli inakuwa salama sana inapokuwa imetia nanga bandarini, ndege inakuwa salama kabisa ikiwa imetua kwenye uwanja wa ndege. Ni mpaka pale meli inapotoa nanga na kuanza kuelea, au ndege inaondoka uwanjani na kuanza kupaa ndipo hatari zinaweza kujitokeza. Kwa meli kukubwa na dhoruba na kuzama au ndege kukutana na hali (more…)

UKURASA WA 1127; Unaanza Na Mtu Mmoja…

By | January 31, 2018

Kuanza jambo lolote jipya, huwa ni kugumu. Hii ni kwa sababu wengi huwa tunafikiria makubwa. Kwamba mtu anapotaka kuanza kitu, anawaangalia wale ambao tayari wameshafanya kwa muda mrefu na kufika juu kabisa. Kwa mfano kama unataka kuanza biashara, halafu unaowaangalia ni wakina Mengi au Bakhresa, utaona kwamba wako mbali sana, (more…)

UKURASA WA 1126; Upendo Na Wema…

By | January 30, 2018

Ukisikie neno Msamaria mwema unapata picha gani? Kwa wengi ni mtu ambaye anajitoa kuhakikisha maisha ya wengine yanakuwa bora zaidi, hata kama hakuna anachonufaika nacho moja kwa moja kwa kufanya hivyo. Sasa zipo zawadi kuu mbili ambazo kila mmoja wetu anazo, lakini namna tunavyozitumia tunatofautiana. Zawadi ya kwanza ni upendo. (more…)

UKURASA WA 1125; Kama Ni Kazi, Tayari Imeshakushinda…

By | January 29, 2018

Tunapokutana na kitu kigumu kwenye maisha, tunasema ni kazi kweli kweli. Hii inaonesha ni kwa namna gani tunaitafsiri kazi kwenye akili zetu, kwamba ni kitu chochote ambacho ni kigumu na ambacho hatupo tayari. Sasa kama chochote unachofanya kwenye maisha yako kinakuwa kazi, unakuwa umeshashindwa kabla hata hujaanza. Ukiangalia watu wa (more…)

UKURASA WA 1124; Hapo Unawapa Watu Nafasi Ya Kukutawala…

By | January 28, 2018

Kuna kutawaliwa kwa nguvu, halafu kuna kutawaliwa kwa hisia. Kutawaliwa kwa nguvu au mabavu kunaweza kuumiza, lakini kunafanyika na mtu mwingine, hivyo angalau unaweza kuwa na mtu wa kumlaumu na hata kupambana kupata uhuru wako. Lakini kutawaliwa kwa hisia, kunaumiza zaidi, ila ubaya ni kwamba, unakuwa umejiweka wewe mwenyewe kwenye (more…)