Category Archives: SIKU 30 ZA MAFANIKIO

Hitimisho La Siku 30 Za Mafanikio; Furaha, Furaha, Furaha….

By | October 1, 2014

Kwa siku 30 zilizopita kila siku ulikuwa unapata makala moja ikielezea mbinu za kufikia mafanikio makubwa kwenye kile unachofanya. Tumejifunza njia za kufikia mafanikio, siri za kufikia mafanikio na utajiri, siri za mafanikio kwa wanawake, siri za mafanikio kwa wanafunzi na hata siri za afya bora ili kufikia mafanikio makubwa. (more…)

SIKU YA 30; Misingi Ya Afya Bora Ili Kufikia Mafanikio.

By | September 30, 2014

Hata uwe na mipango mikubwa na mizuri kiasi gani ya kufikia mafanikio, kama hutakuwa na afya nzuri ni vigumu sana kuweza kufikia mafanikio makubwa. Na kama kwenye safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio utaisahau afya yako, hata ukifanikiwa halafu afya yako ikawa mbaya hutaweza kuyafurahia mafanikio yako. Ili kuweza kufikia (more…)

SIKU YA 29; Sheria Ya Uvumilivu Na Ung’ang’anizi Ili Kufiki Mafanikio Makubwa.

By | September 29, 2014

Kitu kikubwa kitakachokufikisha kwenye mafanikio sio muda, juhudi au uwezo. Kitakachokuwezesha kufikia mafanikio makubwa ni msukumo wa ndani ambao unaendeshwa na uvumilivu. Msukumo huu na uvumilivu ndio unaokuwezesha kutumia muda, juhudi na hata uwezo wako mkubwa kufikia mafanikio makubwa. Kuna vikwazo vingi sana kwenye safari ya mafanikio, bila ya uvumilivu, (more…)

SIKU YA 28; Sheria Ya Kujiamini Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | September 28, 2014

Ni hali ya kusikitisha kwamba kushindwa kujiamini kumewazuia watu wengi sana kuweza kufikia mafanikio makubwa. Kutokujiamini ni kikwazo kikubwa kwa watu wengi kufikia mafanikio, ni sehemu ndogo sana ya watu walioweza kufikia mafanikio makubwa ni hii ni kwa sababu wanajiamini. Kutokujiamini ni kukosa imani kwako binafsi na kwenye uwezo wako. (more…)

SIKU YA 27; IMANI, Nguzo Muhimu Sana Ya Kufikia Mafanikio.

By | September 27, 2014

Vitu vyote vina mizizi yake kwenye imani. Kila kitu tunachofanya kwenye maisha kinaanzia na imani. Tunaamini kwamba chakula tunachokula kitaenda kujenga miili yetu na hivyo kutupatia afya bora japokuwa hatujui inatokeaje. Tunaamini kwamba hewa tunayovuta ina mchanganyiko mzuri ambao unahitajika kwenye miili yetu kwa ajili ya kutupatia nguvu. Tunaamini kwamba (more…)

SIKU YA 26; Tabia Za Mafanikio Kwa Wanafunzi.

By | September 26, 2014

Ni vyema kukumbuka kwamba pale tabia za mafanikio zinapokuwa zimejengwa zitaendelea kuwa na wewe mpaka utakapojenga tabia nyingine. Tabia za mafanikio utakazojifunza sasa ukiwa mwanafunzi zitakusaidia katika maisha yako ya elimu na hata maisha yako baada ya elimu. Hizi hapa ni baadhi ya tabia za mafanikio kwako mwanafunzi. 1. Tengeneza (more…)

SIKU YA 25; Siri Za Mafanikio Kwa Wanafunzi.

By | September 25, 2014

Kila mtu anapenda kufanikiwa kwenye maisha yake. Na hata kwa wanafunzi, unapokuwa masomoni unapenda kufanikiwa kufikia viwango fulani ulivyojipangia. Unapenda kupata ufaulu mzuri katika masomo na pia unapenda kupata kazi nzuri baada ya kumaliza masomo yako. Yote haya yanawezekana kwako na kwa kila mwanafunzi kama ataijua misingi muhimu ya kufikia (more…)

SIKU YA 24; Mbinu Za Mafanikio Kwa Wanawake.

By | September 24, 2014

Jamii nyingi zimekuwa zinamuweka mwanamke katika nafasi ya chini sana ya kuweza kufikia mafanikio. Ukiangalia nchi zote duniani, na hata makampuni makubwa sana duniani ni machache sana ambayo yanaongozwa na wanawake. Hata katika biashara za kawaida, viongozi wengi wa biashara ni wanaume. Pamoja na harakati nyingi ambazo zimefanyika kuinua hali (more…)

SIKU YA 23; Siri Ya Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | September 23, 2014

Ukiacha uwezo na nguvu za kawaida ambazo tunazo, kila mtu ana nguvu kubwa sana kupitia mawazo yake. Una nguvu zenye uwezo mkubwa wa kiakili ambazo zinaweza kukufikisha kwenye mafanikio makubwa. Kwa kifupi kila mtu ni ‘genius’ yaani una akili nyingi sana ambazo hujaweza kuzitumia bado. Ubongo wa binadamu una seli (more…)

SIKU YA 22; Akili Yako Ya Ndani Inaweza Kukufikisha Kwenye Mafanikio Makubwa.

By | September 22, 2014

Ni kweli kwamba kuna nguvu kubwa sana ya uumbaji katika akili yako ya ndani(subconscious mind) ambayo inaweza kukuletea chochote unachotaka. Nguvu hii ni kubwa kama ile inayodhaniwa kuwa nguvu ya majini katika hadithi za Allannin, ambapo unasema kitu na kinatokea. Leo tutajifunza jinsi unavyoweza kutumia nguvu hii kufikia mafanikio makubwa. (more…)