Category Archives: BIASHARA NA UJASIRIAMALI

BIASHARA LEO; Vitu Ambavyo Havilipi Moja Kwa Moja Kwenye Biashara Yako.

By | February 26, 2018

Kuna tabia moja ya waajiriwa ambayo nimekuwa naona inawarudisha nyuma sana kwenye kupiga hatua kwenye kazi hiyo. Tabia hiyo ni kufanya yale ambayo wanalipwa tu. Kama mtu halipwi moja kwa moja kwa kufanya kitu, basi hakifanyi. Na utawasikia kabisa wakijiambia kwani nalipwa? Tabia hii nimekuwa naiona pia kwa wafanyabiashara ambao (more…)

BIASHARA LEO; Kwa Nini Mitandao Ya Kijamii Haina Faida Kubwa Kwako Kibiashara Kama Unavyodhani.

By | February 16, 2018

Kwenye zama hizi za taarifa, wateja wanapaswa kuwa na taarifa sahihi za biashara yako ili waweze kuchukua hatua ya kuja kununua kwako. Na moja ya njia rahisi za kutoa taarifa za biashara yako ni kupitia mitandao ya kijamii. Kwa sasa karibu kila mtu mwenye simu, yupo kwenye mitandao hii ya (more…)

BIASHARA LEO; Usiache Kutumia Nguvu Hii Ya Mahusiano Kwenye Biashara Yako…

By | February 12, 2018

Mahusiano yana nguvu kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Tunasukumwa kuchukua hatua pale ambapo mtu ambaye tuna mahusiano naye ana uhitaji au matatizo yanayohitaji msaada wetu. Katika mahusiano, kuna yale ya moja kwa moja, kama ya undugu, ambayo mtu hachagui. Kama mmezaliwa pamoja tayari mna uhusiano, na hivyo (more…)

BIASHARA LEO; Anza Na Wazo Na Hatua Ya Kuchukua.

By | November 6, 2017

Kila mtu anayetaka kuingia kwenye biashara, huwaangalia wafanyabiashara wakubwa ambao wamepata mafanikio makubwa kibiashara. Watu wanapowaangalia wafanyabiashara hawa, huwa wanakwama kuanza kwa sababu hawaoni ni namna gani wanavyoweza kuanzisha biashara inayoweza kuwa kubwa kama za wale wanaowaangalia. Wengi husubiri mpaka wapate wazo ambalo ni kubwa na linaloweza kuzalisha biashara kubwa (more…)

BIASHARA LEO; Ni hatua zipi zitakazofuata kwenye biashara yako?

By | October 30, 2017

Kitu kigumu kwa wengi huwa kimekuwa ni kuingia kwenye biashara. Wengi wanapata shida wakati wa kuchagua biashara gani wafanye na wapate wapi mtaji. Wakishavuka hatua hiyo na kuweza kuanza biashara, wengi huishia hapo. Biashara zao zinabaki kwenye ngazi ile ile ambayo walianzia na hazikui zaidi. Wanaendesha biashara zao kwa mazoea (more…)

BIASHARA LEO; Kila Msaidizi Wako Kwenye Biashara Anapaswa Kujibu Swali Hili Kwa Ufasaha…

By | October 18, 2017

Kumekuwa na changamoto kubwa kwenye kupata wasaidizi wa biashara wenye uwezo mzuri wa kufanya kazi kwenye biashara. Uaminifu na kujituma ni vitu ambavyo vinakosekana kwa wengi tunaowapata watusaidie kwenye biashara zetu. Pamoja na changamoto kuwa kwenye tabia za watu, lakini sisi wamiliki wa biashara pia tuna mchango katika hilo. Kuna (more…)

BIASHARA LEO; Kuvumilia Na Kuridhika Kunaua Biashara Nyingi Sana.

By | October 16, 2017

Kwenye maisha, huwa tunapata kile ambacho tupo tayari kukivumilia. Ndiyo maana unaweza kukuta mtu ana hali ngumu, na angeweza kuchukua hatua kuwa bora ila hafanyi hivyo kwa sababu anaweza kuvumilia hali hiyo ngumu. Angekuwa hawezi kuvumilia, angeshachukua hatua kuondokana na hali hiyo. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye biashara, biashara yetu (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Inaanza Kushindwa Ndani Na Siyo Nje…

By | October 13, 2017

Katika wakati wowote ule, huwa kuna mabadiliko yanayoendelea kwenye uchumi wa nchi na hata dunia kwa ujumla. Kuna wakati uchumi unakuwa vizuri na kuna wakati uchumi unakuwa vibaya. Kuna wakati watu wana uwezo mzuri wa kununua na kuna wakati ambapo watu hawana uwezo wa kununua. Haya ni mambo ambayo yamekuwa (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kutumia Makosa Yako Kibiashara Kujenga Imani Ya Wateja Kwako…

By | October 11, 2017

Bilionea Bill Gates amewahi kuandika kwenye moja ya vitabu vyake kwamba mteja ambaye hajaridhishwa ni sehemu kubwa sana ya kujifunza kwenye biashara. Akiwa na maana kwamba, kama kuna mteja ambaye hajaridhishwa na huduma au bidhaa uliyomuuzia, ni mteja ambaye atakufundisha mengi sana. Ni jambo lisilo na shaka kwamba katika kuwahudumia (more…)

BIASHARA LEO; Mshauri Muhimu Kuhusu Huduma Kwa Wateja Kwenye Biashara Yako Ni Huyu…

By | October 9, 2017

Huwa nasema mtu wa kwanza kuchukua ushauri wake kuhusu wateja wa biashara yako ni wewe mwenyewe. Na unafanya hivyo kwa kuangalia huduma unazopata kutoka kwa wafanyabiashara wengine pale unapokwenda kupata huduma mbalimbali, hata kama haziendani na biashara yako. Kila mmoja wetu, huwa anapata hisia fulani anapokwenda kwenye biashara nyingine. Huenda (more…)