Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1136; Wakati Sahihi Wa Kupambana Na Kudai Kilicho Chako…

By | February 9, 2018

Kuna wakati kwenye maisha watu watakuonea, ni mara nyingi na inaweza kutokea kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako. Lakini huwezi kupambana na kila anayekuonea kila wakati. Kuna wakati kwenye maisha, watu watachukua sifa kwenye kazi ambayo umeifanya wewe. Unakuwa umekazana kweli na kazi hiyo, umeweka nguvu, muda na ujuzi wako, (more…)

UKURASA WA 1135; Ujasiri Ni Uvumilivu…

By | February 8, 2018

Kuna watu ambao tukiwaangalia kwa nje tunasema watu hawa ni jasiri, tunatamani tungekuwa na mioyo kama yao, mioyo ambayo haiogopi chochote na inaweza kuchukua hatua hatari bila ya hofu. Tusichokiona ni kwamba, wale ambao kwa nje tunawaona ni jasiri sana na hawana hofu, ndani yao wana hofu kubwa. Wana hofu (more…)

UKURASA WA 1134; Mamilioni Ya Watu Wameshafanya…

By | February 7, 2018

Kuna wakati unataka kufanya kitu, lakini unakuwa umekwama, ukiwa hujui ufanyeje, au uanzie wapi, au panakuwa na changamoto ambazo hujui utawezaje kuzitatua. Wengi hapa hujiambia haiwezekani na hawawezi kufanya, na kila kitu kinaishia hapo. Ukweli ni kwamba, chochote ambacho unafikiria kufanya lakini hujui ufanyeje, mamilioni ya watu walishakifanya. Wapo watu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JIJUE KISHA JITUMIE…

By | February 7, 2018

Know, first, who you are, and then adorn yourself accordingly. – Epictetus Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa nafasi hii nzuri sana ya leo. Ni fursa ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Ni kwa msingi NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda (more…)

UKURASA WA 1133; Nje Hakubadiliki, Bali Ndani…

By | February 6, 2018

Kuna watu wanaamini dunia ni sehemu ya mateso, sehemu ngumu na yenye kila aina ya shida. Na tangu wanapoamka mpaka wanaporudi kulala, hicho ndiyo wanachoona na kupata kwa siku nzima. Kwa mfano mtu anataka kuwahi mahali, halafu akakutana na foleni kubwa, au chombo alichokuwa anatumia kikaharibika. Hapa moja kwa moja (more…)

UKURASA WA 1132; Badili Stesheni Ya Mawazo…

By | February 5, 2018

Ukiwa unasikiliza redio, labda kuna kipindi kizuri ulikuwa unasikiliza, halafu kikaisha na kikaja kipindi kingine, ambacho siyo kizuri kwako huwa unafanya nini? Je unakaa na kuanza kulalamika kwa nini redio hiyo imeleta kipindi ambacho siyo kizuri wakati wewe unataka kusikiliza vipindi vizuri? Kama akili yako iko sawa huwezi kufanya hivyo. (more…)

UKURASA WA 1131; Kabla Hujabadili Unachofanya…

By | February 4, 2018

Umewahi kusikia kitu kipya kikakuhamasisha sana kuchukua hatua, na ukajiambia utabadilika, na kweli siku chache za kwanza ukawa umebadilika lakini baadaye ukarudi kwenye tabia zile zile za awali? Umewahi kutamani sana kubadili kile unachofanya, ukataka ufanye kazi bora kabisa, utoe thamani kubwa kwa wengine lakini ukajikuta unaishia kufanya yale uliyozoea (more…)