Category Archives: NENO LA LEO

Jifunze kila siku kupitia usemi mbalimbali.

UKURASA WA 148; Mambo Kumi(10) Unayotakiwa Kubadili Leo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | May 28, 2015

Kuna picha moja ya katuni ambapo kiongozi amesimama jukwaani na anawauliza wananchi, wangapi wanataka mabadiliko? Wote wananyoosha mikoni. Anauliza swali la pili wangapi wanataka kubadilika? Hakuna hata mmoja ananyoosha mkono. Hivi ndivyo maisha ya watu wengi yalivyo, kila mtu anataka mabadiliko, anataka maisha yake yawe bora, anataka kuwa na kazi (more…)

UKURASA WA 139; Huyu Ndio Mtu Pekee Anayeweza Kukunyanyasa.

By | May 19, 2015

Kuna wakati unaweza kuona kama watu wengine wanakunyanyasa au kukushambulia kutokana na hali uliyonayo au kitu unachofanya. Katika hali kama hii unachukua hatua gani? Unalalamika kwa nini watu wakushambulie wewe? Unajiona kama ni mtu mwenye bahati mbaya kutokana na hali ulizo nazo ambazo zinawafanya wengine wakunyanyase na kukushambulia? Kama hiki (more…)

UKURASA WA 133; Neno Lako Kama Sheria.

By | May 13, 2015

Mara nyingi watu wamekuwa wakijiuliza kama kile wanachofanya ndio sahihi kwao na kwa jamii nzima inayowazunguka. Na kama mtu hana kipimo kizuri cha kujua kama anachofanya ni sahihi au la, basi anaweza kufanya mambo ambayo yatakuwa na madhara kwake na kw amaisha ya wengine. Leo nakushirikisha njia rahisi ya kujua (more…)

UKURASA WA 118; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka…

By | April 28, 2015

Kuna watu huwa wanasema kwamba siku zao zina kisirani, wengine husema wameamkia upande mbaya na maneno mengine mengi yanayoashiria kwamba kuna siku mbaya na siku nzuri. Tuchukue mfano, umeamka asubuhi na kwa bahati mbaya umeamka kwa kuchelewa, hivyo unaanza kujiandaa haraka haraka, unavaa nguo huku unafanya mambo mengine ili tu (more…)

NENO LA LEO; Tulichozaliwa Nacho Na Tulichojifunza….

By | April 26, 2015

Love is what we were born with. Fear is what we learned here. -Marianne Williamson Upendo ndio kitu ambacho tulizaliwa nacho. Hofu ni kitu ambacho tumejifunza hapa duniani. Upendo utakuletea furaha kwenye maisha, upendo utakuwezesha kufanya kile unachopenda na kufanikiwa na upendo utakuwezesha kuishi na wengine vizuri. SOMA; Hivi Ndivyo (more…)

NENO LA LEO; Ufunguo Mkuu Wa Furaha.

By | April 25, 2015

Love is the master key that opens the gates of happiness. -Oliver Wendell Holmes Upendo ndio ufunguo mkuu unaofungua milango yote ya furaha. Umesoma vizuri hapo juu, upendo ndio ufunguo wa furaha, sio fedha nyingi, sio umiliki wa mali za kifahari na sio kutoka kwa mtu. Kama unataka kuw ana (more…)

NENO LA LEO; Hakuna Uhaba Wa Fursa, Kuna Uhaba Wa Kitu Hiki…

By | April 24, 2015

There is no scarcity of opportunity to make a living at what you love; there’s only scarcity of resolve to make it happen. -Wayne Dyer Hakuna uhaba wa fursa za kutengeneza kipato kwenye kile unachopenda; kuna uhaba wa wewe kuamua kufanya hivyo. SOMA; Njia Ya Uhakika Ya Kufikia Mafanikio Makubwa. (more…)

NENO LA LEO; Kila Kinachotoke Kwenye Maisha Yako Ni Fursa Ya Mambo Haya Mawili.

By | April 23, 2015

I believe that every single event in life happens in an opportunity to choose love over fear. -Oprah Winfrey Naamini kwamba kila tukio linalotokea kwenye maisha ni fursa ya kuchagua kati ya upendo au woga/hofu. Kila tukio linalotokea kwenye maisha yako, linaweza kukupeleka mbele au linaweza kukurudisha nyuma. Hii itatokana (more…)

NENO LA LEO; Najua Umeshasikia Hili Mara Nyingi, Sio Vibaya Ukasikia Tena Na Leo.

By | April 22, 2015

I know you’ve heard it a thousand times before. But it’s true – hard work pays off. If you want to be good, you have to practice, practice, practice. If you don’t love something, then don’t do it. -Ray Bradbury Najua umeshasikia hili mara elfu moja kabla. Lakini ni kweli- (more…)