Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (365/366); Kubali udogo wako.

By | October 31, 2022

#SheriaYaLeo (365/366); Kubali udogo wako. Tulipokuwa watoto tulijua udogo wetu na kukubali kuna mengi ambayo yapo nje ya uwezo wetu. Sasa tumekuwa watu wazima na kusahau udogo huo, kwa kudhani kila kitu kinapaswa kuwa ndani ya uwezo wetu. Lakini ukiuangalia ukubwa wa ulimwengu, sisi bado ni wadogo sana. Ukiangalia umri (more…)

#SheriaYaLeo (364/366); Tafakari maajabu ya dunia.

By | October 30, 2022

#SheriaYaLeo (364/366); Tafakari maajabu ya dunia. Kila unachokiona kwenye maisha yako hapa duniani ni maajabu. Ukianza na mwili wako mwenyewe, una maajabu mengi ambayo huwezi kuyaelezea. Hujui chanzo cha hisia zako, huwezi kuona ubongo wako wala jinsi chakula kinavyomeng’enywa tumboni kwako. Lakini hayo yote yanaendelea kwenye mwili wako na unayaona (more…)

#SheriaYaLeo (363/366); Anga na nyota.

By | October 29, 2022

#SheriaYaLeo (363/366); Anga na nyota. Kwenye usiku usio na mawingu, liangalie anga na utaziona nyota nzuri ambazo zinalipendezesha anga. Ukiangalia anga wakati wa mchana utaliona jua ambalo ni nyota iliyo karibu zaidi na dunia na ambayo mwanga wake unaipa uhai dunia. Bila ya mwanga wa jua, kusingeweza kuwa na maisha (more…)

#SheriaYaLeo (362/366); Penda asili.

By | October 28, 2022

#SheriaYaLeo (362/366); Penda asili. Kuna mambo mengi kwenye maisha yetu ambayo hayapo ndani ya udhibiti wetu. Tunakutana na maumivu, magonjwa, kutengana na hata kifo. Tunakutana na magumu, changamoto na hata kushindwa kwenye mambo mangi ambayo tunapanga kufanya. Tunaweza kufanya kila kitu kwa usahihi kabisa lakini bado tukakutana na hali hizo. (more…)

#SheriaYaLeo (361/366); Tumia vizuri ubongo wa dunia.

By | October 27, 2022

#SheriaYaLeo (361/366); Tumia vizuri ubongo wa dunia. Ubongo ni kiungo chenye nguvu kubwa kwenye miili yetu. Kina nguvu ya kutuwezesha kupata chochote tunachotaka. Kile ambacho tunakifikiri kwa muda mrefu ndiyo kinakuwa uhalisia wetu, kwa sababu ubongo unatuletea taarifa za aina hiyo zaidi. Pamoja na nguvu hiyo kubwa ya ubongo, bado (more…)

#SheriaYaLeo (360/366); Hili nalo litapita.

By | October 26, 2022

#SheriaYaLeo (360/366); Hili nalo litapita. Sisi binadamu huwa tunapenda sana uhakika wa mambo. Hilo ndiyo limekuwa linasababisha tukae kwenye mazoea. Huwa tunataka mambo na hali ziendelee kuwa vile ambavyo zimekuwa. Ndiyo maana mara nyingi huwa tunasema afadhali ya jana. Ukweli ni kwamba, kila kitu kinabadilika. Hakuna kitu chochote ambacho hakibadiliki (more…)

#SheriaYaLeo (359/366); Jiweke kwenye uwanja wa kifo.

By | October 25, 2022

#SheriaYaLeo (359/366); Jiweke kwenye uwanja wa kifo. Tangu enzi na enzi, majenerali wa majeshi wamekuwa wakitafuta njia ya kuwasukuma wanajeshi wao kupambana kwa kila namna ili kupata ushindi. Wapo ambao wamekuwa wakitunia maneno ya hamasa ili kuwahamasisha wanajeshi wao kupambana. Maneno hayo yamekuwa na mafanikio kiasi lakini nguvu yake huwa (more…)

#SheriaYaLeo (358/366); Epuka ukuaji wa kiroho feki.

By | October 24, 2022

#SheriaYaLeo (358/366); Epuka ukuaji wa kiroho feki. Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo kwenye zama hizi ni wengi kushindwa kujua njia sahihi za ukuaji wa kiroho. Lengo la dini lilipaswa kuwa njia ya watu kupata ukuaji wa kiroho. Lakini kwa zama hizi, dini zimeshindwa kuwasaidia watu kwenye hilo. Badala yake zimewajaza hofu (more…)

#SheriaYaLeo (357/366); Ujinga wa kiwango cha juu.

By | October 23, 2022

#SheriaYaLeo (357/366); Ujinga wa kiwango cha juu. Binadamu tunazaliwa, kuishi na kufa. Hivyo ndivyo maisha yamekuwepo tangu enzi na enzi na ndiyo imewezesha dunia kuendelea kuwepo. Viumbe wanaokufa wanatoa nafasi kwa wengine wanaozaliwa. Baadhi ya watu wanatafuta teknolojia ya kurefusha maisha au kuondoa kabisa kifo. Huu ni ujinga wa hali (more…)