Category Archives: UJUMBE WA LEO

Pata ujumbe mzuri kila siku kwa njia ya picha na maneno.

Huoni Fursa Za Mafanikio Kwa Sababu Hii Kubwa.

By | August 19, 2015

Tunaona kile ambacho tunataka kuona, kile ambacho kimejaa kwenye akili zetu na mawazo yetu. Kama akili yako na mawazo yako yamejaa habari za kushindwa basi kila utakachokiangalia utaona kushindwa. Ukiwa na mawazo ya mafanikio kila utakachoangalia utaona mafanikio. Tatizo sio kile unachoangalia, bali tafsiri ambayo tayari unayo kwenye mawazo yako. (more…)

Unategemea Ulipwe Kwa Muda? Hiyo ilikuwa Mwaka 47, Amka.

By | August 7, 2015

Hakuna atakayekulipa kwa sababu tu umekuwa kwenye kazi muda mrefu au kwa sababu unaonekana unafanya kazi muda mrefu. Utalipwa kulingana na thamani unayozalisha. Ukilazisha thamani kubwa unapata malipo makubwa. Kama unazalisha thamani ndogo, au huzalishi kabisa thamani, unategemea nini? Leta mabadiliko leo, fanya kitu kwa utofauti na hakikisha unaongeza thamani. (more…)

Usilalamike, Dunia Imekupa Kila Kitu, Ni Wewe Tu…

By | August 6, 2015

Dunia imeshakupa kila kitu ambacho wewe unataka. Kama unabisha angalia ni watu wangapi ambao wameanzia pabaya kuliko wewe lakini wameweza kufika mbali. Sasa na wewe unawezaje kufika mbali zaidi ya ulipo sasa? Acha kulalamika kwamba dunia haina usawa, Acha kulalamika kwamba kuna wengine wanapendelewa, Amua ni kitu gani unachotaka kwenye (more…)

Kama Unayapigania Mafanikio, Watu Watakuchukia, Usiumizwe na Hilo.

By | August 5, 2015

Wakati wewe unakazana kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio, kuna watu watakuchukia bila sababu yoyote ile. Wakati wao wanapoteza muda na wewe ukaacha kupoteza nao muda, watakuchukia. Wakati wao wanafanya matumizi makubwa kuliko vipato vyao na wewe ukakwepa hilo, watakuchukia. Wakati wao wanafanya kazi kwa kawaida tu na hawamalizi mpaka (more…)

#UJUMBE_LEO; Watu Watano Wa kuambatana nao Na Watu Watano Wa Kuwakimbia Haraka.

By | August 4, 2015

Wote tunajua kwamba maisha yako ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka. Kama watu watano wanaokuzunguka wanakukatisha tamaa na kukutudisha nyuma huwezi kufanikiwa hata ukiwa na juhudi kiasi gani. Kama watu watano wanaokuzunguka wanakupa moyo na kukusaidia ni lazima utafanikiwa. Fanya hilo zoezi hapo juu na hakikisha unawakata watu watano leo (more…)

UJUMBE LEO; Unataka Kupata Fursa Nzuri? Mbinu Ni Hii Hapa.

By | August 2, 2015

Mara nyingi watu wamekuwa wakijikuta kwenye wakati mgumu sana. Hii ni baada ya kuingia kwenye fursa ambayo waliambiwa ni nzuri ila wanapoingia wanakutana na changamoto nyingi sana. Fursa nzuri sana ni ile ambayo unaitengeneza mwenyewe, au unaitafuta mwenyewe na unaweza kuifanya kwa utofauti. Kama fursa umeisikia kwa wengi mara nyingi (more…)