Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1014; Dhambi Kubwa Siyo Kukosea, Bali Kutokufanya Kabisa…

By | October 10, 2017

Karibu kila mtu ana mpango fulani ambao anataka kuufanyia kazi kwenye maisha yake. Watu wengi wanajua nini wanapaswa kufanya kwenye maisha yao, kazi yao, biashara yao na maeneo mengine. Na hata wasiojua, wana wazo kwamba pale walipo sasa bado hapawatoshi na kuna mambo yanayofanywa na wengine ambayo wanatamani na wao (more…)

BIASHARA LEO; Mshauri Muhimu Kuhusu Huduma Kwa Wateja Kwenye Biashara Yako Ni Huyu…

By | October 9, 2017

Huwa nasema mtu wa kwanza kuchukua ushauri wake kuhusu wateja wa biashara yako ni wewe mwenyewe. Na unafanya hivyo kwa kuangalia huduma unazopata kutoka kwa wafanyabiashara wengine pale unapokwenda kupata huduma mbalimbali, hata kama haziendani na biashara yako. Kila mmoja wetu, huwa anapata hisia fulani anapokwenda kwenye biashara nyingine. Huenda (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Uliza Maswali Makuu.

By | October 9, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to tje utmost / Ronald Gross. UKURASA 51 – 60 Socrates alisifika kwa kuwa mtu wa kuhoji. Hakuwa mtu wa kukubali chochote anachoambiwa na kukipokea kama ndiyo kitu kamili. Badala yake alihoji zaidi na zaidi kuhakikisha anaupata ukweli wenyewe. (more…)

UKURASA WA 1013; Uaminifu Unavyojengwa…

By | October 9, 2017

Umewahi kusikia mtu anasema anapenda sana watu wamwamini lakini hawafanyi hivyo? Au huenda wewe mwenyewe, kuna watu unataka sana wakuamini, lakini wao hawana imani juu yako. Labda ni wateja wako, mwajiri wako, mwenza wako, na hata watu wengine wanaokuzunguka. Uaminifu ni kitu muhimu sana kwa mafanikio, kama watu hawakuamini, huwezi (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Kujua imani yako hasa, jiulize kwa nini mara nyingi.

By | October 8, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 37 – 50. Socrates alikuwa akishangaa sana jinsi gani watu hawapendi kufikiri. Alisema watu wengi wanapenda kuamini kile walichopokea na wasikihoji. Pale mtu anapojaribu kuhiji na kuona imani yake inatikiswa, anaacha (more…)

UKURASA WA 1012; Vitu Viwili Utakavyoenda Navyo Kaburini…

By | October 8, 2017

Nimewahi kukuandikia siku za nyuma kwamba wapo watu ambao wanaishi na sisi hata baada ya kufa. Hawa ni watu ambao tunawakumbuka na kutumia mifano yao kwenye maisha yetu ya kila siku. Licha ya wao kuondoka hapa duniani, lakini ipo alama waliiacha ambayo tunaitumia mpaka sasa. Yawezekana watu hawa ni watu (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jijue Wewe Mwenyewe…

By | October 7, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 27 – 36. Kupitia mtindo wake wa mijadala, Socrates anatufundisha ya kwamba, zoezi muhimu sana ambalo kila mtu anapaswa kufanya ni kujijua yeye mwenyewe kwanza. Anasema watu wengi hukimbilia kuomba ushauri (more…)