Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; KUJUA CHA KUFANYA NA KUFANYA UNACHOJUA…

By | October 7, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Ni siku nyingine nzuri sana na ya kipekee ambapo tumepata fursa nyingine nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya (more…)

UKURASA WA 1011; Matokeo Ya Kujiweka Wewe Mbele Ya Wengine…

By | October 7, 2017

Kwa asili sisi binadamu ni wabinafsi, na ubinafsi wetu umetuwezesha kuona hatari mbalimbali na kuendelea kuwepo mpaka sasa. Lakini ubinafsi wetu huu unaweza kuwa kikwazo kikubwa kwenye maisha yetu kama hatutauelewa haraka na kuchukua hatua. Kwa kawaida watu hujiangalia wao wenyewe kwanza, kwenye kila jambo, lazima mtu aangalie usalama wake (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Mtindo wa kufundisha wa Socrates na kwa nini hakuandika kitabu.

By | October 6, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. Ukurasa; 17 – 26. Pamoja na ushawishi mkubwa ambao Socrates amekuwa nao kwenye falsafa zote duniani, Socrates hakuwahi kuandika kitabu chochote. Hakuna kitabu chochote ambacho kimeandikwa na Socrates. Socrates aliamini kwamba, njia (more…)

UWEKEZAJI LEO; Tofauti Ya Mbahatisha Hisa Na Mlanguzi Hisa Kwenye Uwekezaji.

By | October 6, 2017

Katika uwekezaji kwenye hisa, kuna nyakati mbili ambazo wawekezaji huweza kutengeneza faida kubwa au kupata hasara kubwa. Nyakati hizi zimekuwa zikisoma uelekeo wa soko na watu kuchukua hatua ambazo zinawanufaisha au kuwapa hasara. Nyakati hizo mbili ni kama ifuatavyo; Mbahatisha hisa (BEAR MARKET). Hii ni hali inayotokea pale bei ya (more…)

UKURASA WA 1010; Hasira Za Kurushiwa…

By | October 6, 2017

Wapo watu ambao wana hasira na maisha yao, lakini hasira hizi hawazielekezi kwao wenyewe, bali kwa wengine. Hivyo kuna wakati unaweza kushangaa mtu anakuwa na hasira na wewe, wakati hakuna jambo lolote baya umemfanyia. Labda tu umemweleza maendeleo yako mazuri, ghafla anabadilika, anaanza kuwa na hasira na wewe na kukukatisha (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; SOCRATES; Menta wa mamenta…

By | October 5, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 6 – 16. Ukiangalia kwa undani falsafa zote za kale, kuanzia Ugiriki mpaka Roma, zina misingi yake kutoka kwa mwanafalsafa Socrates. Socrates anaweza kuchukuliwa kama mwasisi wa misingi mingi ambayo falsafa nyingi (more…)

BIASHARA LEO; Wateja Wako Wanatamani Sana Kitu Hichi Kimoja Kutoka Kwako…

By | October 5, 2017

Mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii imempa kila mtu sauti, kila mtu sasa anaweza kuongea, kila mtu anaweza kutangaza chochote na kuwafikia watu wengi zaidi. Kibiashara hili limeleta changamoto mpya kwa wateja. Wanasikia kelele nyingi sana kiasi kwamba wanashindwa kujua wachukue hatua gani. Pale kila mtu anapoongea na kuahidi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MISINGI YAKO ITAJARIBIWA…

By | October 5, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni fursa nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo mazuri sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na (more…)

UKURASA WA 1009; Matokeo Ni Muhimu Zaidi Kuliko Maelezo…

By | October 5, 2017

Kama unataka kuwashawishi watu kufanya kitu, kuchukua hatua fulani ambayo unaamini ni muhimu na bora kabisa kwao, unaweza kutumia njia mbili. Njia ya kwanza ni kuwaeleza kwa kuwaambia kipi wanapaswa kufanya. Kuwaeleza kwa kina kila hatua wanayopaswa kuchukua. Na ili kuhakikisha wanahamasika hasa kuchukua hatua, itakuhitaji kukamata hisia zao pia. (more…)