Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2280; Kila kitu kinaanza na mteja…

By | March 29, 2021

2280; Kila kitu kinaanza na mteja… Watu huwa wanahangaika na mambo mengi kwenye biashara zao, ambayo hata siyo muhimu. Yale ya muhimu kabisa na yanayoiwezesha biashara kupiga hatua huwa hayapewi uzito mkubwa. Watu huhangaika na wazo, jina, mtaji, eneo na mengine, lakini mteja hawampi kipaumbele kikubwa. Watu huhangaika na mbinu (more…)

2279; Maswali matano muhimu ya kukupa mwanga…

By | March 28, 2021

2279; Maswali matano muhimu ya kukupa mwanga… Kuna wakati unaweza kujiona kama umepoteza uelekeo katika kufanyia kazi ndoto zako. Ni katika wakati huo unahitaji kuwa na kitu kinachokupa mwanga ili ujue vipi vipaumbele sahihi kwako. Hapa kuna maswali matano muhimu ambayo ukijiuliza na kujipa majibu, utapata mwanga mkubwa. 1. Nini (more…)

2278; Mafanikio makubwa yanayaka usiwe wa

By | March 27, 2021

2278; Mafanikio makubwa yanayaka usiwe wa kawaida… Huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kuwa mtu wa kawaida, kufanya yale wengine wanafanya kwa namna ambayo wengine wanafanya. Yaani ulishajiona tu watu wanakuelewa, sahau kuhusu mafanikio, kwa sababu hakuna kikubwa na cha tofauti utakachokuwa unafanya. Ili upate mafanikio makubwa, lazima ufanye kitu ambacho (more…)

2276; Kamata tamaa zao…

By | March 25, 2021

2276; Kamata tamaa zao… Huwa hatuzipendi hisia hasa wakati wa maamuzi, lakini hatuwezi kufanya maamuzi yoyote bila hisia. Hili limethibitishwa kisayansi, baadhi ya watu waliofanyiwa upasuaji wa ubongo na eneo la hisia kuharibiwa, waliweza kufikiri vyema kabisa, lakini hawakuweza kufanya maamuzi. Chukua mfano mtu anaenda kwenye mgahawa na kuangalia vyakula (more…)

2275; Mambo sita muhimu kwenye ushawishi…

By | March 24, 2021

2275; Mambo sita muhimu kwenye ushawishi… Mafanikio yako yanategemea sana ushawishi wako, hivyo ni muhimu uwe na ushawishi mzuri. Katika kuboresha ushawishi wako, zingatia haya sita. 1. Uharaka, watu huwa hawasukumwi kuchukua hatua kama kitu hakina uharaka. Ndiyo maana siku ya mwisho ya kufanya kitu ndiyo wengi hufanya. Hivyo weka (more…)

2274; Kushindwa kwa kujitakia…

By | March 23, 2021

2274; Kushindwa kwa kujitakia… Ukianzisha ugomvi na mtu, wewe ndiye unayeshindwa. Kwa sababu kwenye ugomvi wowote ule, kuna kushinda na kushindwa. Iwapo utashindwa, hapo iko wazi umeshindwa, kwa ugomvi ulioanzisha wewe mwenyewe. Na iwapo utashinda, bado wewe ndiyo umeshindwa, kwa sababu umejishusha kwenye ngazi ya chini kwa yule uliyeshindana naye. (more…)

2273; Marudio…

By | March 22, 2021

2273; Marudio… Kumbuka wimbo ambao unaupenda sana, umeusikiliza au kuuangalia mara ngapi? Kumbuka chakula unachokipenda sana, umekila mara ngapi kwenye maisha yako? Kumbuka somo ambalo umewahi kufaulu kuliko mengine ulipokuwa shuleni, ulilisoma mara ngapi? Yale yote muhimu na unayoyapenda, umekuwa unayarudia rudia kila mara. Mziki unaoupenda huwa unausikiliza au kuuangalia (more…)

2272; Kama hutaki matusi yakuumize…

By | March 21, 2021

2272; Kama hutaki matusi yakuumize… Kama matusi ya wengine yakuumize, usikubali pia sifa wanazokupa zikuvimbishe kichwa. Mara nyingi watu wanapotusifia na kutuambia maneno mazuri tunafurahi na kujisikia vizuri. Lakini watu wanapotutukana au kutukosoa tunachukia na kujisikia vibaya. Hali zote tunazitengeneza sisi wenyewe na wala siyo maneno wanayotoa wengine. Unapofurahishwa na (more…)

2271; Kazi zako ni mbili, pesa na madili…

By | March 20, 2021

2271; Kazi zako ni mbili, pesa na madili… Kinachofanya biashara nyingi ndogo kutokukua ni wamiliki wa biashara hizo kufanya kazi ndani ya biashara badala ya nje ya biashara. Kufanya kazi ndani ya biashara ni kufanya kile ambacho hata ukimwajiri mtu anafanya. Yake majukumu ya kila siku ya biashara husika. Tatizo (more…)