Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2315; Uchoshi Ndiyo Mafanikio…

By | May 3, 2021

2315; Uchoshi Ndiyo Mafanikio… Kama huwezi kuukubali uchoshi (boredom) na kuishi nao, huwezi kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Mafanikio ni marudio ya muda mrefu ya vitu vinavyoboa. Wengi hufikiri mafanikio ni matokeo ya tukio moja kubwa la kishujaa, lakini sivyo. Fikiria kwenye fedha, wengi tunapenda hadithi za mtu aliyetoka (more…)

2313; Maamuzi Ya Kamati…

By | May 1, 2021

2313; Maamuzi Ya Kamati… Huwa kipo kichekesho kwamba kamati ni kikundi cha watu wasio na uwezo na ambao hawapo tayari waliopewa jukumu lisilokuwa muhimu. Maamuzi yanayofanywa na kamati ni yale ambayo mtu mmoja hataki kulaumiwa kwa maamuzi anayofanya. Hilo hupelekea maamuzi yanayofikiwa na kamati kuwa ya kubembelezana na siyo yanayosimamia (more…)

2312; Ukishafanya Maamuzi…

By | April 30, 2021

2312; Ukishafanya Maamuzi… Kinachofuata ni kuyatekeleza, kujifanyia tathmini na kuboresha kadiri unavyokwenda. Na siyo kuanza kuyahukumu maamuzi yako mwenyewe baada ya kuwa umeyafanya, hata kama umekosea kwenye kuyafanya, kujihukumu haitasaidia. Bali unapaswa kujitathmini na kuyaboresha. Pia siyo kupoteza muda kutaka kila mtu aelewe na kukubaliana na maamuzi hayo. Wengi hawataelewa (more…)

2311; U mpweke…

By | April 29, 2021

2310; U mpweke… Umewahi kutamani watu wakione kitu kwa namna fulani unavyokiona wewe lakini wanashindwa kufanya hivyo? Umewahi kuwa na hisia fulani kwenye jambo lakini wengine wakawa na hisia tofauti unayoshindwa kuielewa? Unapojikuta kwenye hali hiyo usione kama una tatizo, bali tambua ndivyo kila mtu alivyo. Kila mmoja wetu anaiona (more…)

2310; Njia ya kupunguza msongo…

By | April 28, 2021

2310; Njia ya kupunguza msongo… Chanzo kikuu cha msongo wa mawazo huwa ni kuyaruhusu mawazo yazurure yatakavyo. Unakuwa unafanya kitu kimoja, ila mawazo yako yako kwenye kitu kingine tofauti kabisa. Kwa mawazo yako kuzurura, yanatengeneza kitu kisichokuwepo, wakati kilicho mbele yako hukofanyi vizuri. Kinachotokea ni muda unakuwa umeisha, umejipa hofu (more…)

2309; Vitu vya kushangaza…

By | April 27, 2021

2309; Vitu vya kushangaza… Waliofanikiwa wanajua kuna mengi hawajui na hivyo kuwa tayari kuendelea kujifunza kupitia kila fursa wanayoweza kuitumia. Ambao hawajafanikiwa wanaamini wanajua kila kitu na hawana haja ya kijifunza, na hivyo hawajifunzi. Matajiri wana fedha nyingi, lakini matumizi yao huwa siyo makubwa. Masikini hawana fedha, ila matumizi yao (more…)

2308; Mambo muhimu ya kujikumbusha…

By | April 26, 2021

2308; Mambo muhimu ya kujikumbusha… Katika safari ya mafanikio, unakabiliana na mambo mengi kiasi kwamba usipojikumbusha yale muhimu unaweza kuyasahau na ukajiingiza kwenye wakati mgumu. Hapa kuna mambo muhimu ya kujikumbusha katika safari hii ya mapambano. Usijiwashe moto ili kuwapa joto wengine. Ni muhimu kuwajali wengine na kuweka maslahi yao (more…)

2307; Wanachokulipa ndiyo thamani yako…

By | April 25, 2021

2307; Wanachokulipa ndiyo thamani yako… Ni kawaida kuwasikia watu walioajiriwa wakilalamika kwamba waajiri wao wanawalipa mshajara kidogo, ambao hauendani kabisa na thamani yao. Pia wapo waliojiajiri na walio kwenye biashara ambao wanalalamika kipato au faida wanayoingiza ni ndogo ukilinganisha na thamani yao. Iko hivi rafiki, kama umeajiriwa na mwajiri wako (more…)