Category Archives: TABIA ZA MAFANIKIO

KUJIAMINI; Umuhimu Wa Tabia Ya Kujiamini.

By | October 14, 2014

Karibu tena msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA katika kipengele hiki cha tabia za mafanikio. Tunaendelea kujifunza tabia ya kujiamini na leo tutajifunza umuhimu au faida ya tabia ya kujiamini. Kujiamini binafsi ni tabia muhimu sana kwenye maisha yako, ni muhimu kuliko unavyofikiri wewe. Tabia hii ya kujiamini ndiyo itakayokuwezesha kufikia (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Kujijengea Tabia Ya Kujiamini.

By | October 7, 2014

Karibu tena msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA kwenye kipengele hiki cha KUJIJENGEA TABIA ZA MAFANIKIO. Kwa miezi mitano iliyopita tumejifunza jinsi ya kujijengea tabia muhimu sana ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Tabia tulizojifunza mpaka sasa ni; tabia ya kujisomea, tabia ya kutumia vizuri muda, tabia ya kutunza na kutumia vizuri (more…)

Uhusiano Wa Nidhamu Binafsi Na Mafanikio Makubwa.

By | September 30, 2014

Mpaka sasa tumeshajifunza nini maana ya nidhamu binafsi, faida zake na hata jinsi ya kujijengea nidhamu binafsi. Pia tumeona kwamba kujenga nidhamu binafsi sio kazi ndogo ila pia sio kwamba haiwezekani. Inahitaji kujitoa na kujipanga ili kuweza kufikia nidhamu binafsi. Nidhamu binafsi ndio hitaji na msingi mkubwa wa kuweza kufikia (more…)

Mambo Muhimu Ya Kuzingati Wakati Wa Kujenga Nidhamu Binafsi.

By | September 23, 2014

Kujenga nidhamu binafsi sio kazi rahisi. Kuna changamoto nyingi sana ambazo utakutana nazo na kama hujajipanga vizuri unaweza kukata tamaa na kuacha kabisa. Wiki iliyopita tulijadili jinsi ya kujenga nidhamu binafsi. Baada ya kujua hayo leo tutajifunza mambo muhimu ya kuazingatia wakati wa kujenga nidhamu binafsi. Hapa kuna mambo matano (more…)

Jinsi Ya Kujenga Nidhamu Binafsi.

By | September 16, 2014

Karibu msomaji kwenye kipengele hiki cha kujenga tabia za mafanikio ambapo mwezi huu wa tisa tunajifunza kuhusu nidhamu binafsi. Kama tulivyoona kwenye makala zilizopita nidhamu binafsi ni uweze wa kufanya jambo unalotaka kufanya bila ya kujali unajisikia kulifanya au la. Pia tuliona nidhamu binafsi ni muhimu sana kwako kuweza kufikia (more…)

Umuhimu na Faida za Nidhamu Binafsi

By | September 9, 2014

Nidhamu binafsi ni moja ya vitu muhimu sana ambapo kila binadamu anapaswa kuwa nacho. Nidhamu binafsi ndiyo inayokuwezesha kufanya maamuzi na kuweza kusimamia maamuzi hayo hata kama mambo yatakuwa magumu kiasi gani. Nidhamu binafsi itakuwezesha kuepuka kuwa na uteja wa tabia fulani, kuondoa uvivu na kukufanya uweze kuendelea kufanya kitu (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Kujenga Tabia Ya NIDHAMU BINAFSI.

By | September 2, 2014

Mpenzi msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA karibu tena kwenye kipengele cha TABIA ZA MAFANIKIO. Katika kipengele hiki kila mwezi tunajadili tabia moja muhimu itakayotuwezesha kufikia mafanikio makubwa. Mwezi wa tano tulijadili tabia ya matumizi mazuri ya muda, mwezi wa sita tukajadili tabia ya kujisomea, mwezi wa saba na wa nane (more…)

FEDHA; Usiifanyie Kazi Fedha, Wacha Fedha Ikufanyie Kazi Wewe.

By | August 26, 2014

Kwa miezi miwili, kila wiki tumekuwa tukipata makala moja ya kujifunza jinsi ya kujenga tabia nzuri kwenye matumizi ya fedha. Pia tumejifunza jinsi ya kujenga tabia ya kujiwekea akiba na muhimu zaidi tumejifunza jinsi ya kuwekeza fedha ili kupata thamani zaidi. Kama umefuatilia makala zote hizi kwa makini na kuanza (more…)

FEDHA; Uwekezaji Wa Fedha Zako Kama Umeajiriwa Au Huna Muda Wa Kutosha.

By | August 19, 2014

Wiki iliyopita katika makala hizi za kujenga tabia za mafanikio, tuliona aina za uwekezaji ambazo mtu aliyejiajiri au anayefanya biashara anaweza kuzifanya. Aina hizo ni zile ambazo zinahitaji muda mwingi wa kufuatilia ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ile isome kwa kubonyeza maneno haya. Leo (more…)

FEDHA; Uwekezaji Wa Fedha Zako Kama Unafanya Biashara au Umejiajiri.

By | August 12, 2014

Wiki iliyopita katika tabia za mafanikio tulijadili umuhimu wa kuwekeza fedha baada ya kuweka akiba kwa muda fulani. Hii inatokana na thamani ya fedha kushuka haraka sana hivyo bila ya kuwekeza unaweza kujikuta unapoteza fedha kwa kuziweka tu benki au kwingine unakuweka. Leo tutaangalia aina mbalimbali za uwekezaji ambapo mtu (more…)