2182; Ni Kwa Sababu Unapenda, Siyo Kwa Sababu Kuna Kitu Unategemea Kupata…

By | December 21, 2020

Chochote unachofanya kwenye maisha kwa mategemeo ya kupata kitu fulani, ukiweka juhudi utapata kile unachotaka kufanya. Lakini ukishakipata, huo ndiyo unakuwa mwisho wako, na wakati mwingine kupata ulichokuwa unatafuta kunaweza kuwa sumu na kikwazo kwako kupiga hatua zaidi. Wale wanaofanikiwa zaidi, wale wanaofanya makubwa kwenye maisha yao, ni wale wanaofanya (more…)

2181; Punguza Maamuzi Unayofanya…

By | December 20, 2020

Kila maamuzi unayofanya, yanapunguza sehemu ya nguvu ya utashi wako wa kiakili. Kadiri unavyofanya maamuzi mengi kwenye siku yako, ndivyo unavyochoka kiakili na kushindwa kufanya maamuzi bora. Na siyo lazima maamuzi yawe makubwa ndiyo yakuchoshe, chochote unachofikiria kwa muda kabla ya kuchukua hatua, kinakula nguvu yako ya akili. Mfano kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MOTO HUMEZA KILA KINACHOWEKWA…

By | December 20, 2020

“What’s thrown on top of the conflagration is absorbed, consumed by it—and makes it burn still higher.” – Marcus Aurelius Moto mkubwa na unaowaka kwa ukali, huwa unageuza kila kinachowekwa kwenye moto huo kuwa nishati na kuwaka zaidi. Moto huo hauogopi chochote unachopokea, badala yake unakipokea na kukigeuza moto unaowaka (more…)

2180; Kama Umeridhika, Inatosha…

By | December 19, 2020

Ni mara ngapi umefanya kazi au jambo ambalo umeridhishwa nalo kweli kweli. Unajivunia kwamba umeweza kufanya kitu ambacho ni tofauti na mazoea, zaidi ya ambavyo umekuwa unafanya. Lakini baadaye mtu mwingine anakuja na kukosoa kile ulichofanya na kukuambia hakuna ulichofanya kabisa, ni kitu cha hovyo. Unakubaliana naye, unajidharau, unaamini kweli (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KURIDHIKA NA KUYAFURAHIA MAISHA…

By | December 18, 2020

“They who have decided to dedicate their lives to spiritual perfection will never be dissatisfied or unhappy, because, all that they want is in their power.” —Blaise Pascal Kama unataka kuridhika na kuyafurahia maisha yako, Basi jitoe kwa ajili ya ukuaji wa kiroho. Unapojitoa kwa ajili ya ukuaji wa kiroho, (more…)

2178; Nunua Kabla Hujauza…

By | December 17, 2020

Watu hawawezi kununua kitu unachouza kama hawajahamasika, Na huwezi kuwahamasisha watu kununua kitu kama wewe mwenyewe hujahamasika, Na zaidi, huwezi kuhamasika kama hujakikubali kweli kile unachouza. Hivyo kama unataka kuuza vizuri kitu, kinunue wewe mwenyewe kwanza, kikubali kweli kweli, hamasika juu ya kitu hicho. Kadiri unavyokuwa umehamasika kuhusu kitu, ndivyo (more…)