#TAFAKARI YA LEO; KUJUA HUJUI…

By | October 23, 2020

“As your island of knowledge grows, so too does the shoreline of ignorance.” – John Wheeler Watu wengi hufikiri lengo la kujifunza ni kujua kila kitu. Kabla hawajaanza kujifunza, huamini wanajua karibu kila kitu. Hivyo wanapoingia kwenye kujifunza, hasa kwa kujisomea vitabu ndiyo wanakutana na ukweli ambao hawajawahi kuujua. Kadiri (more…)

2122; Kutafuniwa…

By | October 22, 2020

Wakati nasoma shule ya sekondari, kwenye somo la Kiingereza kulikuwa na vitabu vya fasihi na ushairi ambavyo vilikuwa kwenye mtaala, ambavyo kila mwanafunzi alipaswa kuvisoma na kwenye mitihani kulikuwa na maswali ya kujibu kutokana na vitabu hivyo. Mwalimu wetu wa Kiingereza alitufundisha vitabu viwili tu na kuamini hivyo vingekuwa msaada (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HATIMA YAKO NI MAAMUZI YAKO…

By | October 22, 2020

“The only person you are destined to become is the person you decide to be.” Ralph Waldo Emerson Watu huwa wanaamini kwamba kila mtu anazaliwa na hatima ya maisha yake. Kwamba mtu anazaliwa akiwa ameshapangiwa kabisa atakuwa na maisha ya aina gani. Wale wanaoamini hivi ndiyo ambao huwa hawaweki juhudi (more…)

2121; Jikinge Na Mihemko Ya Wengine…

By | October 21, 2020

Watu wengi huwa wanaendesha maisha yao kwa hisia, kwa kufuata mihemko yao. Ndiyo maana wengi hawawezi kufanya maamuzi na kuyasimamia kwa muda mrefu. Ni sawa na mtu anayeenda kwenye mkutano wa hamasa au kusoma kitabu cha hamasa, anahamasika sana na kutoka akiwa anajiambia anakwenda kubadilika na kufanya makubwa. Lakini anapolala (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KILA KINACHOTOKEA KITAKUWA NA MATUMIZI KWAKO…

By | October 21, 2020

Do not be concerned too much with what will happen. Everything which happens will be good and useful for you. — Epictetus Mtu mmoja alipotelewa na farasi aliyekuwa anamtegemea sana, majirani zake wakaja kumpa pole kwa upotevu huo. Siku chache baadaye farasi aliyepotea akarudi akiwa na farasi wengine wawili wa (more…)

2120; Kazi Na Mbwembwe…

By | October 20, 2020

Watu wamekuwa wanatumia nguvu nyingi kwenye mbwembwe kuliko kwenye kazi. Kwenye maonesho kwamba wanafanya kazi kuliko kazi yenyewe wanayoifanya. Wengi wanakazana ili waonekane wanafanya kazi, ili waonekane wako ‘bize’ lakini hakuna chochote kikubwa wanachozalisha. Na haya yote yamechochewa na ukuaji wa mitandao ya kijamii, maana hiyo inampa kila mtu nafasi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO UNACHOPATA, BALI UNACHOTOA…

By | October 20, 2020

“When you approach a man, you should think not about how he can help you, but how you might serve and help him.” – Leo Tolstoy Mara nyingi unapokutana na mtu huwa unaangalia anawezaje kukusaidia badala ya kuangalia unawezaje kumhudumia. Hata kwenye kazi na biashara, unaangalia nini unachopata na siyo (more…)

2119; Kuna Gharama Zaidi Utakayoilipa…

By | October 19, 2020

Kila unapoendelea kusubiri na usianze kufanya kile ulichopanga kufanya, kuna gharama ya zaidi ambayo utalazimika kuilipa. Kila unaposubiri mpaka tarehe ya mwisho ya kufanya kitu ikaribie ndiyo ufanye, utakifanya kwa haraka na ubora utakuwa hafifu kitu ambacho kitakugharimu zaidi au kukupunguzia manufaa ambayo ungeyapata kama ungekifanya mapema. Kila unaposubiri mpaka (more…)

2118; Kujikana Wewe Mwenyewe…

By | October 18, 2020

Wanaotaka mafanikio makubwa ni wengi, Wanaotaka kuwa na utajiri ni wengi, Wanaotaka umaarufu ni wengi, Lakini ni wachache sana wanaopata kile wanachotaka, katika watu 100 ni mmoja pekee anayefikia kile hasa anachotaka. Siyo kwa sababu watu hao ni wa tofauti sana, ila watu hao wamejitoa zaidi ya wale ambao hawafikii. (more…)