2127; Tunaomba Upokee Pesa Zetu…

By | October 27, 2020

Fikiria upo kwenye biashara na umefika hatua ambayo badala wewe uwabembeleze wateja wanunue, wateja wanakubembeleza wewe upokee pesa zao, ukubali kuwauzia kile unachouza. Unafikiri hizo ni ndoto? Ni uhalisia kabisa, biashara zote ambazo zimeweza kufikia mafanikio makubwa, zimeweza kufika hatua hiyo ya wateja kubembeleza kuuziwa, wateja wanaiomba biashara ipokee pesa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KITAKACHOBADILI MAISHA YAKO…

By | October 27, 2020

“Life will only change when you become more committed to your dreams than you are to your comfort zone.” – Bill Cox Maisha yako yatabadilika pale utakapojitoa zaidi kwa ajili ya ndoto zako kubwa kuliko kujitoa zaidi kwenye mazoea. Vita ya kwanza na kubwa kabisa unayopaswa kuishinda ni kuachana na (more…)

2126; Dagaa Siyo Watoto Wa Samaki Wakubwa…

By | October 26, 2020

Ukiwaangalia dagaa na kuwalinganisha na samaki wengine wakubwa, unaweza kufikiri dagaa ni watoto wa samaki, ambao kama wangeachwa basi wangekuja kuwa samaki wakubwa. Lakini huo siyo ukweli, dagaa ni jamii ya samaki ambao ni wadogo, hivyo unapomuona dagaa ni samaki aliyekamilika, hata aachwe kiasi gani, hatafikia ukubwa wa samaki wengine (more…)

2125; Kutafuta Sababu Za Kushindwa…

By | October 25, 2020

Kwa kuwa mafanikio ni magumu kupatikana na kwa kuwa kwenye mambo mengi ambayo mtu anaanza kufanya atashindwa, wengi wamekuwa wanatengeneza mazingira ambayo yatawapa sababu za kushindwa. Mfano mzuri ni kipindi ukiwa shule, japokuwa unajua una mtihani, unaweza usisome au usome kwa kujificha ili matokeo yanapotoka na ukawa hujafanya vizuri basi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAJALI MAONI YA NANI?

By | October 25, 2020

“It never ceases to amaze me: We all love ourselves more than other people, but care more about their opinion than our own.” — Marcus Aurelius Kila mtu huwa anajipenda mwenyewe kuliko anavyowapenda wengine. Hii ndiyo njia pekee iliyotuwezesha sisi binadamu kufanikiwa. Maana kwa kujipenda na kujijali, inakuwa rahisi kuwapenda (more…)

2124; Tabia Zinapiga Kelele Kuliko Maneno…

By | October 24, 2020

Nina rafiki yangu mmoja ambaye tunajuana kwa karibu miaka kumi sasa. Ni rafiki ambaye haipiti muda sijakutana naye na mara nyingi huwa ni kwa kutembelea ofisi yake. Siku za karibuni, amepata rafiki mwingine ambaye wanashirikiana naye kwenye ofisi yake. Hivyo ninapoenda pale ofisini kwa rafiki yangu, nakutana na huyo mwingine (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAVUNA ULICHOPANDA…

By | October 24, 2020

“Whatever we plant in our subconscious mind and nourish with repetition and emotion will one day become a reality” — Earl Nightingale Watu huwa wanayalalamikia maisha yao wakiamini kuna watu wamepelekea wao kufika pale walipo sasa. Lakini ukweli ni kwamba popote mtu alipo, ni mavuno ya kile alichopanda kwenye fikra (more…)

2123; Ni Bora Kufanya Bure Kuliko Kutokufanya Kabisa…

By | October 23, 2020

Upo usemi wa Kiswahili kwamba mtembea bure siyo sawa na mkaa bure, maana yule anayetembea bure anaweza kukutana na fursa ambazo anayekaa mahali pamoja bure hawezi kuzipata. Kauli hii inahusika kwenye maeneo mengi ya maisha yetu, ikiwepo kazi zetu mbalimbali. Mtazamo mkuu tulionao kwenye shughuli mbalimbali tunazofanya ni kulipwa kadiri (more…)