2628; Ndiyo biashara yenyewe.

By | March 12, 2022

2628; Ndiyo biashara yenyewe. Sisi binadamu huwa tunafanya vitu kwa misukumo ya hisia mbili; tamaa na hofu. Huwa tunafanya kitu kama kuna kitu kizuri tunapata (tamaa) au kama hatutaki kupoteza tulichonacho (hofu). Kwa kujua hili, inakusaidia sana kuelewa kwa nini baadhi ya watu huwa wanafanya vitu ambavyo hukutegemea wafanye. Unaweza (more…)

#SheriaYaLeo (132/366); Angalia tabia wanazoficha.

By | March 12, 2022

#SheriaYaLeo (132/366); Angalia tabia wanazoficha. Katika kuchagua watu wa kushirikiana nao, huwa tunaamini haraka kile ambacho tunasikia na kuona kwao. Tunaamini hivyo ndivyo watu walivyo na yale wanayotuambia na kutuonyesha ndiyo uhalisia wao. Tunachosahau ni kila mtu kuna tabia anazo ambazo huwa hapendi kuziweka wazi. Huenda hata yeye mwenyewe hajui (more…)

#SheriaYaLeo (131/366); Usichanganye kujiamini kulikopitiliza na ukweli.

By | March 11, 2022

#SheriaYaLeo (131/366); Usichanganye kujiamini kulikopitiliza na ukweli. Sisi binadamu huwa tunadanganyika kirahisi sana. Pale mtu anapotueleza kitu kwa kujiamini sana, huwa tunaona ni ukweli, kwamba kama isingekuwa kweli basi wasingejiamini. Hii ndiyo njia wanayotumia matapeli na watu wengine wenye lengo la kudanganya na kuhadaa kwa manufaa yao. Huwa wanaeleza jambo (more…)

#SheriaYaLeo (130/366); Tambua mlipuko wa kihisia.

By | March 10, 2022

#SheriaYaLeo (130/366); Tambua mlipuko wa kihisia. Pale mtu anapopata mlipuko mkali wa kihisia dhidi yako, mfano hasira ambayo haiendani na kile ulichofanya, tambua ni mbinu ya kutaka kukutawala kihisia. Wapo watu ambao hutumia mlipuko wa hisia kuibua hisia kali ndani yako ili waweze kukutawala. Wanajua ukishakuwa na hisia kali, huwezi (more…)

2625; Usife.

By | March 9, 2022

2625; Usife. Katika safari ya mafanikio ya mtu yeyote yule, bahati ina mchango wake. Kila historia ya aliyefanikiwa, kuna mahali alikutana na bahati au fursa ya kipekee na ikampa manufaa makubwa. Kinachowatofautisha wanaokutana na bahati na ambao hawakutani nazo siyo bahati yenyewe, bali muda. Yaani siyo kwamba kuna watu wana (more…)

#SheriaYaLeo (129/366); Angalia mapito yao.

By | March 9, 2022

#SheriaYaLeo (129/366); Angalia mapito yao. Kiashiria kizuri cha tabia za watu ni mapito yao. Kwa kuangalia historia zao na yale ambayo wamefanya huko nyuma, unaweza kupata picha ni watu wa aina gani. Watu wanaweza kusema wamejifunza na kubadilika kutokana na yale waliyopitia, lakini siyo rahisi hivyo. Kuna tabia huwa zinaendelea (more…)

2624; Kanuni ya heshima au imani.

By | March 8, 2022

2624; Kanuni ya heshima au imani. Watu wamekuwa wanalalamika kwamba hawaheshimiwi au hawaaminiwi. Lakini ukiangalia kwa uhalisia, tatizo huanzia kwa watu kutokujiheshimu au kujiamini wenyewe. Leo napendekeza kanuni rahisi ambayo ukiifuata utajijengea heshima kubwa na kuaminika na wengine. Kanuni hiyo inakwenda hivi; Heshima/imani = utekelezaji/ahadi Ili heshima au imani iwe (more…)

#SheriaYaLeo (128/366); Wanaotumia udhaifu kukutawala.

By | March 8, 2022

#SheriaYaLeo (128/366); Wanaotumia udhaifu kukutawala. Kuna watu huwa wanatumia udhaifu walionao kukutawala wewe bila ya mwenyewe kujua. Wanakuwa na tabia fulani sugu ambayo inakukwamisha wewe, lakini unapojaribu kuwakabili kwenye tabia hiyo wanajionyesha hawana hatia na wewe ni mtu mbaya na usiyejali. Wanaweza kuwa na tabia sugu ya kuchelewa kila wakati. (more…)