2623; Gharama zilipojificha.

By | March 7, 2022

2623; Gharama zilipojificha. Kipo kichekesho kinaeleza mgahawa ambao ulitumia mbinu ya masoko kuwashawishi wateja kununua kwa wingi. Mgahawa huo uliweka tangazo kwa nje likieleza; kula leo watalipa wajukuu wako. Watu walivutiwa na hilo na kuingia kuagiza chakula. Baada ya kula wahudumu waliwaletea bili. Hapo ndipo wateja wakawa wanagoma kwamba tangazo (more…)

#SheriaZaLeo (127/366); Unachoona siyo uhalisia.

By | March 7, 2022

#SheriaZaLeo (127/366); Unachoona siyo uhalisia. Watu huwa wanatumia mwonekano wa nje kuwahadaa wengine. Pale wanapokuwa na udhaifu fulani, huwa wanatengeneza mwonekano unaoficha udhaifu huo. Lengo lao ni kuwanasa wengine kwa namna ambayo wao watanufaika zaidi. Wewe kuwa makini usinase kwenye mitego huo. Jua siyo kila unachoona kwa nje ndiyo uhalisia (more…)

2622; Sababu zipo tayari.

By | March 6, 2022

2622; Sababu zipo tayari. Kama unataka kufanya kitu, au hutaki kukifanya, sababu zipo tayari. Kama utafanikiwa au utashindwa, sababu zipo tayari. Yaani sababu tayari ziko mbele yako, ni wewe tu uchague unataka nini, halafu uchukue sababu zinazoendana na kile unachotaka. Kama unataka kweli kupata kitu, sababu za kukitaka tayari unazo. (more…)

#SheriaYaLeo (126/366); Kuwa makini na watu unaowachokoza.

By | March 6, 2022

#SheriaYaLeo (126/366); Kuwa makini na watu unaowachokoza. Watu huwa wanabadilika, hakuna anayebaki pale alipoanzia. Mtu anaweza kuwa chini leo, lakini siku zijazo akawa juu kabisa. Hivyo kuwa makini sana na watu unaowachokoza, kuwadharau au kuwatukana. Leo anaweza asiwe na nguvu ya kukufanya chochote, lakini siku zijazo akawa na nguvu na (more…)

2621; Machache kuhusu wewe yanawatosha.

By | March 5, 2022

2621; Machache kuhusu wewe yanawatosha. Sisi binadamu tuna kasumba moja, kadiri tunavyokijua zaidi kitu ndivyo tunavyokichukulia kawaida na kukidharau. Lakini pale tunapokuwa hatukijui sana kitu huwa tunakiheshimu na kukichukulia kwa uzito mkubwa. Kwa kujua hili, wawekee watu mipaka ya kujua kuhusu mambo yako. Kadiri watu wanavyojua machache kuhusu maisha yako (more…)

#SheriaYaLeo (125/366); Usidanganyike na mwonekano wa nje.

By | March 5, 2022

#SheriaYaLeo (125/366); Usidanganyike na mwonekano wa nje. Mara nyingi watu wamekuwa wanatengeneza mwonekano fulani wa nje ambao unaficha nia yao halisi. Kwa nje wanaigiza kama wajinga na wasiojua vitu fulani. Lengo lao ni kuwahadaa watu ili wasijue nia zao na kuwa kikwazo kwao. Wewe kuwa makini, usikimbilie kuamini mwonekano wa (more…)

2620; Matumaini na uhakika.

By | March 4, 2022

2620; Matumaini na uhakika. Watu huona matumaini kama kitu cha kujifurahisha, ambacho siyo uhalisia. Hupenda zaidi uhakika kwenye kila jambo. Lakini ukweli ni kwamba katika hali ya kawaida, kuujua ukweli ni vigumu sana. Hivyo kujipa uhakika kabla hujaujua ukweli ni kujiweka kwenye hatari kubwa, kuwa kikwazo kwako mwenyewe kupiga hatua. (more…)

#SheriaYaLeo (124/366); Wahukumu kwa tabia zao, siyo maneno yao.

By | March 4, 2022

#SheriaYaLeo (124/366); Wahukumu kwa tabia zao, siyo maneno yao. Kwenye safari yako ya mafanikio na maisha kwa ujumla, jifunze kutokudanganyika na maneno ambayo watu wanakuambia, badala yake angalia tabia wanazokuonyesha. Watu husema maneno ya kila aina na kujaribu kuficha nia zao halisi kwa maneno mazuri. Lakini matendo yao huwa hayadanganyi, (more…)

2619; Siyo hawamudu, bali hawajali.

By | March 3, 2022

2619; Siyo hawamudu, bali hawajali. Kama unauza kitu, iwe ni bidhaa au huduma na wateja uliowapata hawapo tayari kulipia, ni rahisi kuona labda hawamudu. Utakimbilia kuona bei ndiyo kikwazo kwao, ni kubwa kwao na hivyo hawamudu. Na wanaweza kukuambia hivyo kweli. Lakini hata utakapojaribu kupunguza bei, bado hawatakuwa tayari kununua. (more…)

#SheriaYaLeo (123/366); Wakabili wanaocheza rafu.

By | March 3, 2022

#SheriaYaLeo (123/366); Wakabili wanaocheza rafu. Katika safari ya mafanikio na maisha kwa ujumla, utakutana na watu ambao wanacheza rafu. Hawa ni wale ambao wapo tayari kutumia kila namna kupata kile wanachotaka. Kwa nje watu hao hujionyesha ni wema, wastaarabu na wanaojali. Ila kwa ndani watu hao ni sumu, wenye mbinu (more…)