Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

1914; Hadithi, Hadithi…

By | March 28, 2020

Kuna sababu kwa nini kila aina ya jamii ina aina zake za hadithi. Hadithi ambazo zimekuwa zinatumika kufundisha maadili na misingi mbalimbali kwenye jamii hizo. Sisi binadamu tunaelewa zaidi kupitia hadithi kuliko maelezo ya kawaida. Pia tunakumbuka zaidi hadithi kuliko tunavyoweza kukumbuka maelezo mengine tunayopewa. Kupitia hadithi, tunauvaa uhusika, na (more…)

1913; Asili Haikufanya Kazi Ya Bure…

By | March 27, 2020

Mmoja wa wanasayansi wa mageuzi (evolution) alifikiria kwamba asili huwa inatengeneza vitu vyenye matumizi. Kama kitu kitatengenezwa halafu kisitumiwe, basi huwa kinapotea. Kwa kufikiri huko, alikuja na dhana kwamba hapo zamani, nyoka walikuwa na miguu, ila kwa kuwa hawakuitumia miguu yao, basi ilipotea. Hakuwa sahihi kwenye nyoka, lakini alikuwa sahihi (more…)

1911; Jipe Muda Wa Kuhofia…

By | March 25, 2020

Hakuna binadamu asiye na hofu, Hofu ni sehemu yetu wanadamu, ndiyo kitu pekee kinachotufanya tuendelee kuwa hai. Siku ambayo utaondoa kabisa hofu zote ulizonazo, ni siku ambayo utakuwa kwenye hatari kubwa. Hofu ni njia ya akili zetu kutuambia tunapaswa kuwa makini zaidi na kitu kwa sababu kuna madhara makubwa mbeleni. (more…)

1910; Usitumie Kuwasaidia Wengine Kama Kisingizio…

By | March 24, 2020

Tabia pekee ya sisi wanadamu ambayo imetupa mafanikio makubwa ni ushirikiano baina ya binadamu. Katika ushirikiano huu, kuna kutoa na kupokea. Kutoa ni sehemu ya ushirikiano huu ambayo inapewa uzito sana, kwa sababu ni rahisi watu kujisahau, wakapokea tu bila kutoa. Hivyo ili kujenga jamii bora, lazima kila mtu awe (more…)

1909; Tatizo Lako Halina Utofauti…

By | March 23, 2020

Ni rahisi kuwapa watu ushauri pale wanapokuwa na matatizo au changamoto fulani. Lakini sisi wenyewe tunapokuwa kwenye tatizo au changamoto hiyo hiyo, hatuwezi kutumia ushauri wetu wenyewe. Hii ni kwa sababu huwa tunajiaminisha kwamba tatizo tulilonalo sisi ni tofauti na matatizo wanayokuwa nayo watu wengine. Lakini huo siyo ukweli, ni (more…)

1908; Siku 100 Za Kwanza…

By | March 22, 2020

Mabadiliko yoyote makubwa unayofanya kwenye maisha yako, siku 100 za kwanza huwa ni siku ngumu sana kwenye mabadiliko hayo. Maisha yatakuwa magumu sana kwenye siku hizo 100 za kwanza, utashawishika sana kurudi kwenye kile ulichozoea, utaona hakuna manufaa kwenye mabadiliko hayo. Na hapo ndipo wanaofanikiwa na wanaoshindwa wanapotengana. Wanaofanikiwa wanaendelea (more…)