#TAFAKARI YA LEO; BILA YA NAMBA…

By | July 17, 2021

Maendeleo na hatua zote ambazo tumepiga kama binadamu, ni kwa sababu ya mamba. Uwezo wa kupima na kulinganisha vitu umekuwa msukumo mkubwa kwetu kufanya vitu kwa utofauti mkubwa. Bila ya namba ni rahisi kujidanganya na kuamini unafanya makubwa. Lakini namba hazidanganyi, kama kitu kimefanyika kinaweza kupimika. Weka imani yako kwenye (more…)

2389; Usimwamini Yeyote Bila Ya Kitu Hiki…

By | July 16, 2021

2389; Usimwamini Yeyote Bila Ya Kitu Hiki… Edward Deming amewahi kunukuliwa akisema; “In God we trust, all others must bring data.” Akimaanisha Mungu pekee ndiye wa kumwamini, wengine wote lazima walete data. Ni kauli rahisi hii, lakini kama ukiielewa na kuiishi, lazima utapiga hatua kubwa kwenye maisha na kile unachofanya. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HITAJI KUU LA MAFANIKIO…

By | July 16, 2021

Unapojifunza kwa wengine waliofanikiwa, haimaanishi uwe kama wao ili ufanikiwe. Njia ya uhakika ya kutokufanikiwa ni kujaribu kuwa kama wengine. Hitaji kuu la mafanikio ni wewe kuwa wewe, kujitambua, kujikubali, kujichagua na kujiamini. Hakuna anayeweza kukushinda wewe kuwa wewe na hapo ndipo ilipo nguvu kubwa kwako ya ushindani na kufika (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia samaki.

By | July 15, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia samaki. Samaki ni moja ya kitoweo muhimu kwenye maisha ya kila siku. Kwa kuwa kadiri watu watakavyoendelea kuwepo wataendelea kula, samaki ni moja ya chakula wanachohitaji. Hapa kuna mawazo kumi ya kuweza kuingiza kipato kupitia samaki. Kufuga samaki na kuwauza kwa ajili ya kula. (more…)

2388; Kwa nini ushauri mwingi wa mafanikio haufanyi kazi…

By | July 15, 2021

2388; Kwa nini ushauri mwingi wa mafanikio haufanyi kazi… Vitabu vilivyoandikwa kuhusu siri za mafanikio ni vingi sana. Hadithi za watu waliofanikiwa ni nyingi. Na mafunzo pamoja na ushauri wa mafanikio vimejaa kila kona. Lakini cha kushangaza, idadi ya wanaofanikiwa inabaki kuwa ni ndogo sana. Sababu kubwa ni moja, mafunzo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; CHAGUA KUWEKEZA VIZURI…

By | July 15, 2021

Muda na nguvu zako ni rasilimali muhimu sana kwako. Namna unavyochagua kutumia rasilimali hizo ni juu yako mwenyewe. Wapo wanaozitumia hovyo na kuzipoteza na wapo wanaozitumia vizuri na kunufaika. Wewe chagua kutumia rasilimali hizo vizuri, kwa kuhakikisha unaziwekeza kwenye kufanya mambo yenye tija kwako na kwa wengine pia. Iwe utachagua (more…)