Karibu rafiki upate kitabu MIMI NI MSHINDI, Ahadi yangu na nafsi yangu. Kitabu mimi ni mshindi kinakuwezesha wewe kuishi maisha ya ushindi, maisha ambayo yanakutofautisha wewe na wengine wengi ambao wanashindwa kufikia mafanikio makubwa.
Ukiangalia maisha ya washindi na maisha ya wale ambao wanashindwa yapo tofauti kabisa. Kuna namna ambavyo washindi wanachukulia mambo yao, wanavyotumia muda wao, wanavyotengeneza mahusiano yao na pia wanavyoshirikiana na wengine. Washindi wana njia tofauti za kuweka malengo ambayo wanayafikia na hivyo kuendelea kuwa washindi.
Kwa bahati mbaya sana maisha haya ya ushindi huwa hayafundishwi kwenye jamii zetu wala kwenye mfumo wetu wa elimu. Na hata wale wachache ambao wameweza kufikia ushindi, siyo wote ambao wana hamasa ya kuweza kuwashirikisha wengine mbinu zao. Kwa kukosa maarifa haya muhimu watu wengi wamekuwa wanafanya makosa ya wazi ambayo yanawazuia kufikia ushindi. Vitu kama uaminifu, matumizi mazuri ya muda, kuwa na shukrani ni vitu ambavyo kwa kawaida huwa hatuvipi uzito, lakini ndiyo vitu vyenye umuhimu mkubwa sana.
Kupitia kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI utajifunza mbinu zote za mafanikio na kazi yako inabaki kuzitumia kwenye maisha yako ili uweze kuwa na maisha ya ushindi.
Mambo gani mapya yaliyopo kwenye kitabu hiki?
Kama umekuwa ukisoma vitabu na makala ninazoandika, utakuwa unajua namna vitabu ninavyoandika vilivyo, sasa kitabu hiki kina haya ya ziada ambayo yatakupa maarifa zaidi na hamasa pia;
1. Kuna shuhuda za watu ambao wameshiriki mafunzo ya semina niliyotoa ya MIMI NI MSHINDI, wakielezea jinsi ambavyo mafunzo waliyopata yamebadili mtazamo wao kuhusu maisha yao na hatua wanazokwenda kuchukua. Kwa kusoma shuhuda hizi utaona ni jinsi gani inawezekana na kwako pia.
2. Kuna mifano halisi ya jinsi ambavyo mimi binafsi nimekuwa natumia mbinu hizi za ushindi unazokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki na zikaniletea matokeo bora. Siishii tu kukuambia mbinu hii ni nzuri, bali nitakuonesha nimewezaje kuitumia mimi binafsi na kuweza kupata matokeo mazuri.
3. Kwenye kila sura kuna zoezi la wewe kufanya, hivyo unapomaliza kusoma sura moja ya kitabu hiki kuna zoezi utapewa la kufanya, zoezi hili linakuwezesha wewe kutumia kile ulichojifunza kwenye maisha yako. hutaishia kuwa na maarifa ya juu juu, badala yake utakuwa na namna ya kuyatumia maarifa hayo ili kupata matokeo bora.
4. Kitabu hiki kimeandikwa kwa nafsi ya kwanza, yaani kitabu kizima ni kama unajiambia wewe mwenyewe. Bada ya jina la kitabu kuwa WEWE NI MSHINDI, kwamba mimi nikuambie wewe, unajiambia wewe mwenyewe kwamba MIMI NI MSHINDI, na kitabu chote kipo hivyo, karibu kila kitu utakuwa unajiambia mwenyewe. Hii ina matokeo bora sana kisaikolojia kwa sababu inasisitiza umiliki wa kile unachojiambia.
5. Mwisho wa kitabu hiki kuna TAMKO KUU LA USHINDI, hapa unajipa tamko la ushindi ambalo lina misingi 20 utakayoisimamia. Kwa kujiambia tamko hili na kulirudia kila siku unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanyia kazi yale uliyojifunza.
Kitabu hiki ni kizuri sana kwako kukisoma, kwani kitakufanya wewe ujishauri mwenyewe njia bora kwako kuchukua ili kufikia ushindi.
Kitabu hiki kinawafaa watu gani?
Kila kitabu kina watu wake, na hakuna kitabu kimoja ambacho kinamfaa kila mtu. Hivyo na kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI ni kwa wale ambao wanataka kuishi maisha ya ushindi, wale ambao wanataka kuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Na mafanikio siyo kifedha pekee, bali kwenye kila eneo la maisha.
Wale ambao wamesharidhika na pale walipo, au wameshajiona wanajua kila wanachotaka kujua, kitabu hiki hakiwafai.
Pia wale ambao hawataki kuwa na maisha ya ushindi, wameshakubali kwamba wao ni wa chini na hakuna kinachoweza kuwatoa pale walipo kitabu hiki hakiwafai.
Lakini wale ambao wamekutana na changamoto kwenye maisha yao na wanaelekea kukata tamaa na kuona mambo hayawezekani, hiki ni kitabu kimoja wanachohitaji kukisoma haraka na kisha kurudi kwenye mapambano yao. Kwa sababu kupitia kitabu hiki utajifunza ni nini kimekufikisha hapo ulipo na namna gani ya kutoka hapo.
Mfumo wa kitabu na namna ya kukipata.
Kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI kipo kwenye mfumo wa softcopy (nakala tete) ambayo unaweza kusomea kwenye simu yako ambayo umekuwa unatumia kusomea makala za AMKA MTANZANIA. Pia unaweza kusomea kwenye tablet kama unayo na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta kama unapendelea hivyo. Hii ni njia rahisi ya kujisomea vitabu na kuweza kutembea navyo popote unapokwenda.
Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email na hivyo unaweza kukipata popote ulipo duniani bila hata ya kutoka hapo ulipo.
Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=). Kupata kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI, tuma fedha tsh elfu 10 kwa MPESA 0755953887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717396253 Majina kwenye namba hizo ni Amani Makirita. Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo yenye jina la kitabu MIMI NI MSHINDI pamoja na email yako na utatumiwa kitabu.
Karibu sana tuongeze maarifa kwa pamoja ili tuweze kuishi maisha ya ushindi yatakayotuwezesha kufikia mafanikio makubwa kwenye kila tunachofanya.
Kumbuka chochote unachotaka kwenye maisha yako kinaanza na wewe mwenyewe. Na ili uweze kuanzisha kile unachotaka unahitaji maarifa sahihi ya kufanya hivyo na sehemu mojawapo ya kupata maarifa haya ni kujisomea vitabu.
Nakutakia kila la kheri katika kutumia maarifa utakayoyapata kwenye kitabu hiki.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,