UKURASA WA 868; Una Uhakika Hawapo Kazini?

By | May 17, 2017

Kuna wakati unaweza kuwa unashangaa sana kwa nini watu wanafanya kile ambacho wanafanya, kumbe ukawa hujui ya kwamba watu hao wapo kazini. Yaani unachoshangaa wao kufanya, ndiyo kazi yao, na ndiyo wanalipwa kwa kufanya kile unachowashangaa wao kufanya.

Au wakati mwingine unawashauri watu kitu lakini hawafuati ushauri wako, au unawaambia na hawasikii. Unakuta wao wapo kazini na kinachowafanya walipwe ni wao kufanya au kukubali kile wanachokubali.

Iko hivi rafiki, ni vigumu sana kumfanya mtu aamini kitu ambacho analipwa kwa kutokukiamini. Sijui umenielewa, yaani kama mtu analipwa kwa kuamini 1 ni sawa na 2, huwezi kumbadili aamini kwamba 1 siyo sawa na 2. Utapoteza muda wako bure, kwa sababu mwenzako yupo kazini na ili alipwe, lazima afanye kazi yake.

SOMA; Watu Wanakuangalia Zaidi Ya Kukusikiliza….

Nakukumbusha hili rafiki, ili wakati mwingine unapowashangaa watu kwa nini wanafanya kile wanachofanya, ukumbuke kuangalia kwanza kama hawapo kazini. Au kama watu unawashauri kitu na hawakifanyi, angalia kwanza isije kuwa wanalipwa kwa kufanya kile unachowashauri wasifanye.

Ni tabia yetu binadamu kufanya kile ambacho kina maslahi kwetu, hivyo kama kitu kina maslahi kwa mtu, atakifanya na kukitetea kwa uwezo wake wote.

Hakikisha watu hawapo kazini kabla hujawashangaa au kuwashauri.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.