Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Barua ya IV; Kuhusu hofu ya kifo.

By | May 26, 2023

Barua ya IV; Kuhusu hofu ya kifo. Rafiki yangu Mstoa,Moja ya hofu ambazo zimekuwa zinatusumbua sana sisi binadamu, ni hofu ya kifo.Sote tunajua kuna siku tutakufa, siku ambayo hatuijui. Lakini kila tunapofikiria kuhusu kifo, huwa tunaingiwa na hofu kubwa. Hofu ya kifo imekuwa moja ya vitu vinavyowazuia watu wasiyaishi maisha (more…)

3068; Kuweka na kutoa.

By | May 26, 2023

3068; Kuweka na kutoa. Rafiki yangu mpendwa,Kuna hadithi nyingi tulizokuwa tunafundishwa tulipokuwa watoto, ambazo zilikuwa na mafunzo makubwa sana kuhusu maisha.Nyingi zilikuwa na mafunzo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wetu kuelewa kwenye hicho kipindi. Kwa mfano kuna hadithi ya kijana ambaye alipewa kazi ya kwenda kulisha mifugo nje kidogo ya (more…)

3067; Imani, Ujuzi, Kazi.

By | May 25, 2023

3067; Imani, Ujuzi, Kazi. Rafiki yangu mpendwa, Kuna kanuni chache sana za mafanikio.Lakini zimekuwa zikipinduliwa pinduliwa na kuishia kuonekana kama ni nyingi na ngumu.Hilo huwa linawakatisha tamaa wengi na kushindwa kufanikiwa. Maneno matatu yaliyopo hapo juu, siyo mageni kuyasikia.Na hata maana za maneno hayo unazijua vizuri kabisa. Lakini leo nataka (more…)

3065; Maumivu hayajatosha.

By | May 23, 2023

3065; Maumivu hayajatosha. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu ni viumbe wa tabia, huwa tunaanza kujenga tabia, kisha tabia zinatujenga.Asilimia kubwa ya yale tunayofanya kila siku, tunayafanya kwa tabia na mazoea na siyo kwa fikra. Hilo ndiyo huleta upinzani mkali sana kwenye mabadiliko.Watu huwa hawapo tayari kuachana na tabia na maumivu yao.Njia (more…)

3064; Usawa usiowezekana.

By | May 22, 2023

3064; Usawa usiowezekana. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu huwa tunapenda sana usawa kwenye kila eneo la maisha.Tunapenda vitu vyote viende sawa ili tuyafurahie maisha yetu.Lakini ukweli mchungu ni kwamba, hakuna usawa kwenye mambo yote na wala hautakuja kuwepo. Mambo yote kwenye maisha huwa yanakwenda kwa kanuni za asili, ambazo haziangalii usawa (more…)

3063; Kataa kushindwa.

By | May 21, 2023

3063; Kataa kushindwa. Rafiki yangu mpendwa,Kitu kimoja ambacho nimekuwa narudia sana kukisema ni kwamba watu huwa hatupati kile tunachotaka, bali kile tunachokubali, tunachokivumilia. Na nimekuwa nikitumia mifano rahisi ya miji mikubwa.Ni vigumu sana ukasikia mtu amekufa kwa njaa kwenye mji wowote mkubwa.Lakini ndani ya miji hiyo, kuna wengi ambao hawana (more…)

3062; Hakuna mjadala.

By | May 20, 2023

3062; Hakuna mjadala. Rafiki yangu mpendwa,Fikiria kuna kitu muhimu sana ambacho unataka kununua.Unaongea na muuzaji wa kitu hicho na anakupa bei.Mnajadiliana kwenye bei na kufikia muafaka kati yako na muuzaji. Unaondoka kwenda kuchukua fedha za kulipia kama mlivyokubaliana.Unarudi ukiwa na kiasi cha fedha kilichokamilika kulingana na makubaliano.Lakini muuzaji anakuambia hataweza (more…)

Barua ya III; Urafiki wa kweli na wa uongo.

By | May 19, 2023

Barua ya III; Urafiki wa kweli na wa uongo. Rafiki yangu Mstoa,Kuna watu ambao huwa tunawachagua wawe karibu yetu kwenye maisha.Watu hao, hatulazimiki kuwa nao kama ilivyo kwa ndugu, bali tunakuwa tumechagua kwa hiari yetu wenyewe kuwa karibu nao.Watu hao ni marafiki. Marafiki ni watu muhimu sana kwenye maisha yetu.Ni (more…)

3061; Kuaminiana.

By | May 19, 2023

3061; Kuaminiana. Rafiki yangu mpendwa,Dunia inaendeshwa kwa msingi mkuu wa kuaminiana.Bila ya kuaminiana, dunia haiwezi kwenda. Tunaweza kufanya yote tunayoyafanya kwenye maisha, kwa sababu tunaweza kuwaamini wengine bila hata ya sababu yoyote. Tunakuwa tayari kuyaweka maisha yetu kwenye hatari kubwa kwa kuwaamini wengine kwamba watafanya kile kilicho sahihi. Fikiria unaenda (more…)