Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; AMINI KWENYE MATENDO…

By | December 13, 2020

“Do not believe in words, yours or others’; believe in the deeds.” – Leo Tolstoy Kusema ni rahisi, Kupanga ni rahisi, Lakini kuchukua hatua kwenye yale ambayo mtu anasema na kupanga siyo rahisi. Hivyo unachopaswa kuamini kwako mwenyewe na hata kwa wengine siyo maneno, bali matendo. Usidanganyike na kile watu (more…)

2173; Kwa Sababu Hawawezi Kuishi Bila Hivyo…

By | December 12, 2020

Kuna mashindano mengi huwa yanaendeshwa kuibua vipaji vya wasanii, yaani kupata wasanii wapya ambao kwa namna fulani hawapati nafasi ya kuonekana. Lakini wasanii wote wakubwa unaowajua, hawajaibuliwa na mashindani ya aina hiyo. Kuna mashindano mbalimbali ya kibiashara huwa yanafanyika, kuibua mawazo ya biashara ambayo watu wanayo na kuwapa nafasi ya (more…)

2172; Uimara Wa Msingi…

By | December 11, 2020

Msingi wa kitu chochote kile, unapaswa kuwa imara, ili kuweza kubeba uzito unaoambatana na kitu hicho. Hivyo uimara wa msingi ndiyo unaopima ukubwa kiasi gani unaweza kufikiwa. Ukichukua mfano wa mimea, miti mikubwa na inayodumu kwa muda mrefu, huwa ina mizizi mikubwa na mirefu, hiyo ndiyo inaipa nguvu, kwa kuhakikisha (more…)

2171; Bila Ya Ukinzani…

By | December 10, 2020

Tusingeweza kutembea duniani, maana tungekuwa tunateleza tu. Tusingeweza kuanzisha moto. Mashine zisingeweza kuwashwa wala kuzimwa. Ndege zisingeweza kupaa angani. Lakini ukinzani huo… Unamaliza soli za viatu, Unafanya vifaa vya mashine viishe haraka, Unapelekea hitaji ya nishati kubwa kuendesha mashine mbalimbali. Unaweza kuona jinsi asili inavyofanya kazi hapo, ukinzani unazuia vitu, (more…)

2170; Unacholalamikia, Unakistahili…

By | December 9, 2020

  Kitu chochote unachokilalamikia au kulaumu kwenye maisha yako, unakistahili kabisa. Na kadiri utakavyoendelea na malalamiko na lawama zako, utaendelea kuwa na kitu hicho. Hakuna namna mambo yataenda kama unavyopanga wewe, hivyo kulalamikia watu au hali fulani kuwa kikwazo kwako ni utoto. Na kama hujui hilo, basi unastahili kabisa kile (more…)

2169; Kikiwa Muhimu, Unawekeza Kweli…

By | December 8, 2020

Kitu kinapokuwa muhimu kwa mtu, hufanya uwekezaji wa kutosha kwenye kitu hicho ili apate matokeo mazuri kwenye kitu hicho. Angalia pale mtu anapoumwa, atafanya awezavyo ili apate matibabu sahihi na aweze kupona. Angalia kwenye harusi, hata kama mtu ni masikini kiasi gani, atapambana awezavyo harusi iweze kwenda vizuri. Atahakikisha gharama (more…)