Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA ASUBUHI; KILA WAZO LINA MADHARA…

By | June 11, 2020

“Every thought a person dwells upon, whether he expresses it or not, either damages or improves his life.” —LUCY MALORY Kila wazo unaloruhusu likae kwenye akili yako, Lina madhara kwenye maisha yako, Iwe utalifanyia kazi wazo hilo au la. Madhara ya wazo yanategemea aina ya wazo lenyewe. Kama wazo ni (more…)

1988; Kosa Siyo Kukosea, Bali Kutokujifunza…

By | June 10, 2020

Tulipozaliwa hatukuwa tunajua kitu chochote kwenye maisha, zaidi ya kulia na kunyonya. Mengine yote tunayojua sasa, tumekuwa tunajifunza. Na kwa kuwa hatujui, katika kujifunza kwetu tumekuwa tunakosea mara kwa mara na makosa hayo ndiyo yanatufanya kuwa bora zaidi. Hukusimama na kuanza kutembea moja kwa moja, bali ulianguka kabla hujajua jinsi (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; KUELEWA PEKEE HAITOSHI, FANYA KITU…

By | June 10, 2020

“It’s not enough to understand; you’ve got to do something.” — Sandra Day O’Connor Umesoma kitabu na kuielewa dhana fulani vizuri, usiishie hapo, fanya kitu kwa dhana hiyo uliyoielewa. Umemsikiliza mtu akifundisha kitu fulani na kuelewa vizuri, usiishie hapo, nenda kachukue hatua mara moja kwa kile ulichoelewa. Unaweza kuelewa vizuri (more…)

1987; Kuwa Sumaku…

By | June 9, 2020

Sumaku ni chuma ambayo imepitia mabadiliko yanayoifanya iweze kuvuta chuma nyingine zinazofanana nayo. Weka plastiki karibu na sumaku na haiwezi kuvuta plastiki hiyo. Lakini weka chuma na mara moja itavutwa. Kuna somo kubwa hapa la kujifunza kuhusu maisha na mafanikio. Kwanza kabisa unahitaji kuwa mtu ambaye anayavutia mafanikio kuja kwako. (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; WATU UNAOPASWA KUJIHUSISHA NAO…

By | June 9, 2020

“Associate with people who are likely to improve you.” — Seneca Watu pekee unaopaswa kujihusisha nao, ni wale ambao wanaweza kukufanya uwe bora kuliko ulivyo sasa. Hawa ndiyo watu wanaoongeza thamani kwenye maisha yako, Watu ambao wanakupa nafasi ya kujifunza kitu kutoka kwao au kupata hamasa ya kupiga hatua zaidi. (more…)

1985; Mkulima Na Mwindaji…

By | June 7, 2020

Mkulima anapaswa kulima shamba, kupanda mazao, kuyapalilia, kuweka mbolea, kupalilia tena na kisha kusubiri yakomae ndiyo ayavune. Kwa njia hii anahitaji kujenga mahusiano ya karibu na kile anachofanya, anapokwenda kulala anafikiria mazao yake, mvua ikiwa nyingi au kidogo anafikiria mazao yake na hili linamfanya ajitoe zaidi na katika kujitoa huko (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; KAMA HUTAKI MAADUI…

By | June 7, 2020

“Be strict in judging yourself and gentle in judging others, and you will have no enemies.” — CHINESE WISDOM Kama hutaki maadui kwenye maisha yako, Kuwa mkali kwenye kujihukumu mwenyewe na mpole kwenye kuhukumu wengine. Sisi binadamu huwa hatuoni kitu kama kilivyo, bali huwa tunakiona kama tunavyokihukumu. Yaani tunaanza kwa (more…)

1984; Kinachokuponza Ni Kulinganisha…

By | June 6, 2020

Dalali akitaka ununue au kulipia kitu, huwa anakutengenezea njia ya kufanya ulinganisho, ambao utakupelekea kufanya maamuzi anayotaka yeye. Chukua mfano unataka kupanga nyumba na unaenda kwa dalali, ambaye unamweleza mahitaji yako kwenye nyumba unayotaka kupanga. Moja kwa moja atajua katika nyumba alizonazo ipi itakufaa. Lakini hatakupeleka kwenye nyumba ile moja (more…)