Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

3295; Ufuatiliaji wa karibu.

By | January 8, 2024

3295; Ufuatiliaji wa karibu. Rafiki yangu mpendwa, Kitu kimoja ambacho nimejifunza kwenye kupata chochote unachotaka ni ufuatiliaji wa karibu unalipa sana. Mara nyingi sana huwa hupati kile unachotaka kwa mara ya kwanza unapokuwa unakitaka.Huwa kuna kizuizi fulani ambacho kinakuwepo. Baada ya kizuizi hicho, kupata au kutokupata unachotaka, huwa kunategemea sana (more…)

3294; Onekana, weka kazi na sikiliza.

By | January 7, 2024

3294; Onekana, weka kazi na sikiliza. Rafiki yangu mpendwa, Kwa kipindi ambacho nimekuwa natoa hii huduma ya mafunzo na ukocha, nimejifunza mengi sana kuhusu watu.Nimejifunza hayo kwa nadharia na kwa vitendo pia kutoka kwenye tabia halisi za watu. Kwenye nadharia nimekuwa najifunza mara kwa mara vitu vitatu vinavyohitajika ili huduma (more…)

3293; Njia ya kuepuka kifo.

By | January 6, 2024

3293; Njia ya kuepuka kifo. Rafiki yangu mpendwa,Kila ambacho kimezaliwa au kuanzishwa, safari yake huwa inaishia kwenye kifo.Hiyo siyo tu kwa viumbe hai, bali kwa vitu vyote. Mwenendo wa kila kitu huwa una mwendo ambao uko dhahiri kabisa. Huo ndiyo mzunguko ambao mtu unapaswa kuutumia vizuri ili kuepuka kifo. Mzunguko (more…)

3292; Kuvutiwa na maneno.

By | January 5, 2024

3292; Kuvutiwa na maneno. Rafiki yangu mpendwa, Maneno huwa ni rahisi sana kuyatoa,Na matendo huwa ni magumu sana kuonyesha.Watu ni rahisi kukupa maneno mazuri na yanayoshawishi.Lakini inapokuja kwenye matendo, wengi huwa siyo watekelezaji wazuri wa yale wanayoongea. Hivyo basi, unapaswa kuwa makini sana na maneno ya watu.Usiyape maneno uzito mkubwa (more…)

3291; Kupambania unachotaka.

By | January 4, 2024

3291; Kupambania unachotaka. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi wamekuwa hawapati kile wanachotaka, siyo kwa sababu hawawezi kupata, bali kwa sababu wanashindwa kukipambania kweli. Kila kitu ambacho mtu anakitaka, kinawezekana kabisa kupatikana.Lakini hakiwezi kupatikana kirahisi.Lazima mapambano makali sana yaweze kuvukwa na yule anayetaka. Ni mapambano makali kwa sababu kuna vikwazo vingi vya (more…)

3290; Unachoshindana nacho.

By | January 3, 2024

3290; Unachoshindana nacho. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi wamekuwa wanalalamikia ushindani kuwa mkali na kuwa kikwazo kwao kufanikiwa kwenye biashara.Wanaona kama isingekuwa ushindani basi wangekuwa wamepiga hatua kubwa sana. Lakini huo siyo ukweli.Kama kuna ushindani pekee ambao unawakwamisha watu kwenye biashara basi ni uvivu na uzembe.Uvivu na uzembe ndiyo vikwazo vikubwa (more…)

3289; Kusubiri kuanza.

By | January 2, 2024

3289; Kusubiri kuanza. Rafiki yangu mpendwa,Kama kuna kitu ambacho unataka kukifanya, lakini kwenye kuanza unasubiri kwanza, hujakitaka kweli kitu hicho. Kadiri unavyosubiri kwa muda mrefu kuanza kufanya kitu, ndivyo inavyokuwa vigumu kuanza kukifanya na hata kupata mafanikio. Hiyo ni kwa sababu kusubiri kunapooza kitu na kuondoa ule msukumo na uharaka (more…)

3288; Hatua unayochukua.

By | January 1, 2024

3288; Hatua unayochukua. Rafiki yangu mpendwa, Kila mtu kuna vitu anavyokuwa anavitaka kwenye maisha yake.Na anaweza kujiwekea malengo na mipango mbalimbali juu ya vitu anavyotaka. Lakini ili mtu aweze kupata kile anachotaka, anapaswa kuchukua hatua kwenye yale anayopanga.Hilo ni la msingi kabisa, lakini limekuwa linapuuzwa na wengi.Wengi wanadhani kupanga na (more…)

3287; Mabadiliko ya watu.

By | December 31, 2023

3287; Mabadiliko ya watu. Rafiki yangu mpendwa, Moja ya vitu vigumu sana kutokea ni watu kubadilila.Mabadiliko huwa ni kitu kigumu sana kwa watu kiasi kwamba ukiona yametokea kweli, basi mtu anakuwa amelipa gharama kubwa sana. Katika hali za kawaida, watu huwa hawabadiliki.Kile ambacho kwa nje tunaweza kuona kama ni mabadiliko (more…)

3286; Kushangazwa na dunia.

By | December 30, 2023

3286; Kushangazwa na dunia. Rafiki yangu mpendwa,Kanuni rahisi ya furaha inahusisha matarajio na uhalisia.Pale matarajio yanapokuwa makubwa kuliko uhalisia, mtu unakosa furaha.Na pale matarajio yanapokuwa madogo kuliko uhalisia, mtu unapata furaha. Inapokuja kwenye matarajio na uhalisia, dunia huwa inatushangaza.Tunapokuza sana kimoja, kingine huwa kidogo mpaka kutushangaza.Hivyo dunia inaweza kutushangaza kwa (more…)