Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; KINATOKEA KAMA KINAVYOPASWA KUTOKEA…

By | February 14, 2018

Everything that happens happens as it should, and if you observe carefully, you will find this to be so. – Marcus Aurelius Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo (more…)

UKURASA WA 1140; Dhana Yako Ya Ubaya Na Uzuri Siyo Sahihi…

By | February 13, 2018

Kuna maeneo ya maisha yetu, ambayo tunajijua hatupo vizuri, lakini sasa si kweli kwamba hatupo vizuri kama tunavyofikiri. Kadhalika yapo maeneo ya maisha yetu ambayo tunajijua tupo vizuri, lakini na hapo pia hatupo vizuri kama tunavyofikiri. Kinachotokea ni kwamba huwa tunajiumiza sana kwa yale maeneo ambayo tunafikiri hatupo vizuri wakati (more…)

BIASHARA LEO; Usiache Kutumia Nguvu Hii Ya Mahusiano Kwenye Biashara Yako…

By | February 12, 2018

Mahusiano yana nguvu kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Tunasukumwa kuchukua hatua pale ambapo mtu ambaye tuna mahusiano naye ana uhitaji au matatizo yanayohitaji msaada wetu. Katika mahusiano, kuna yale ya moja kwa moja, kama ya undugu, ambayo mtu hachagui. Kama mmezaliwa pamoja tayari mna uhusiano, na hivyo (more…)

UKURASA WA 1139; Faida Ya Kuchukua Hatari Kwenye Maeneo Madogo Ya Maisha Yako…

By | February 12, 2018

Kama kuna mambo makubwa ambayo unataka kufanya kwenye maisha yako, ambayo yanakutaka uchukue hatari kubwa, na hilo linakupa hofu, basi njia mbadala ni kuchukua hatari ndogo ndogo kwenye maisha yako. Sisi binadamu ni viumbe wa mazoea, huwa tunafanya zaidi kile tulichozoea kufanya kuliko ambacho hatujazoea. Hivyo unapojifunza kuchukua hatari ndogo (more…)

UKURASA WA 1138; Kwa Nini Akili Yako Haiwezi Kuona Tatizo…

By | February 11, 2018

Umewahi kuona mtu ambaye ana tatizo au anakosea na kila mtu anaona hivyo lakini yeye haoni kabisa? Hata akiambiwa anakataa kabisa, kwa kuamini yupo sahihi? Au wewe mwenyewe, umeshawahi kuwa unafanya kitu ukiona upo sahihi kabisa na watu wanakuonesha mambo yaliyo wazi lakini huoni. Ila baadaye unakuja kugundua kwamba hukuwa (more…)

UKURASA WA 1137; Usikodishe Utu Wako Kwa Wengine…

By | February 10, 2018

Kwenye zama hizi za taarifa, ambapo mitandao ya kijamii imekuwa na nguvu kubwa kwenye maisha yetu, kitu kinachoumia sana kwenye maisha ya wengi ni utu, ile hali ya kujithamini kama mtu, ambayo inaanzia ndani ya mtu mwenyewe. Hali hii inaumia kwa sababu watu hawawezi tena kujithamini wenyewe, bali kusubiri mpaka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUJIFUNZA UNACHOJUA…

By | February 10, 2018

If you desire to be good, begin by believing that you are wicked. – Epictetus Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa nafasi hii nyingine nzuri sana kwetu, nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuishi kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana. Kwa mwongozo wa (more…)