Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Ndani yetu tuna kitu kikubwa, tumekamilika na tuna kila tunachohitaji.

By | October 4, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 227 – 236. Falsafa zote na hata imani za kidini, zinaweka mkazo kwenye kitu kimoja, kwamba sisi ni zaidi ya hii miili tunayoiona. Ndani yetu kuna kitu kikubwa sana, ambacho ndiyo kinabeba (more…)

UWEKEZAJI LEO; Vodacom Wametangaza Kutoa Gawio La Kwanza Kwa Wawekezaji.

By | October 4, 2017

Moja ya faida za kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa ni kupata gawio pale kampuni inapopata faida. Kampuni inawalipa wanahisa wake sehemu ya faidia iliyopata, huku wakiendelea kubaki na hisa zao. Yaani ni sawa na kuweka mtaji kwenye biashara, na ukapata faida huku mtaji wako ukiendelea kuwepo. Kampuni ya Vodacom Tanzania, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAULI CHANYA YA KUIANZA SIKU…

By | October 4, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Ni siku nyingine nzuri sana ya leo, ambapo tumepata nafasi bora na ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya (more…)

UKURASA WA 1008; Maisha Ni Mlolongo Wa Miradi…

By | October 4, 2017

Huwa tunakazana sana kutafuta kanuni moja ya maisha ambayo tukiijua basi maisha yetu yataweza kwenda kwa urahisi, kila kitu kitaenda kama tunavyotaka. Habari mbaya ni kwamba, hakuna kitu kama hicho, hakuna namna tunaweza kuwa na kanuni ya aina hiyo. Hakuna namna tunaweza kujihakikishia kupata kila tunachotaka, kwa wakati ambao tunataka. (more…)

BIASHARA LEO; Maswali Matatu Muhimu Kujiuliza Kuhusu Wateja Wa Biashara Yako.

By | October 3, 2017

Mambo yanabadilika kwa kasi sana, na biashara nazo hazijaachwa nyuma. Kuweza kupona kibiashara kwenye zama hizi za mabadiliko, lazima uwe mbele ya mabadiliko. Lazima uweze kubadilika kabla mabadiliko hayajafika. Tabia za watu zinabadilika sana kwa sasa, na hii inakufanya wewe mfanyabiashara kuzielewa tabia za wateja wako, ili uweze kuwahudumia vizuri (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MATARAJIO NA UHALISIA…

By | October 3, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo ambapo tumepata nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo (more…)

UKURASA WA 1007; Tamaa Ya Kukata Tamaa Na Kuacha…

By | October 3, 2017

Huwa tunaweka mipango mikubwa na mizuri sana ya maisha yetu. Tunapanga nini tunafanya na tunachukua hatua ya kufanya. Lakini tunapoanza kufanya, tunakutana na kitu ambacho hatukutegemea, ugumu, vikwazo na changamoto. Hali hizo tunazokutana nazo, zinatusababishia maumivu ambayo yanaweza kuwa ya mwili au akili, safari inakuwa ngumu kwetu kuliko tulivyotegemea. Ni (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Je kuna kifo kizuri?

By | October 2, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 217 – 226… Wanafalsafa wa kigiriki waliamini kwamba kifo ni zoezi la kiimani. Waliamini maisha yote tunayoishi, ni kujiandaa na zoezi kuu ambalo ni kifo. Socrates alisema falsafa ni kujiandaa na kifo. (more…)

UWEKEZAJI LEO; Faida Tano Za Kuwekeza Kwenye Hatifungani.

By | October 2, 2017

Moja ya uwekezaji kwenye masoko ya mitaji ni kununua hatifungani, ambapo unaikopesha fedha kampuni au taasisi kwa makubaliano ya kulipwa kwa riba. Watu wengi wamekuwa hawaelewi vizuri uwekezaji huu wa hatifungani, kwa sababu hauongelewi sana na kwa hapa Tanzania, hatifungani zinazopatikana sokoni siyo nyingi kama hisa. Leo nakwenda kukushirikisha faida (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIKU YOYOTE NI SIKU YA KUANZA…

By | October 2, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Ni siku nyingine nzuri sana hii, ambapo tumepata nafasi nzuri na ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya (more…)