Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2630; Udhaifu wako mwenyewe.

By | March 14, 2022

2630; Udhaifu wako mwenyewe. Matatizo na changamoto nyingi vimekuwa vinajirudia kwa watu, kwa sababu huwa hawakubali chanzo cha hayo. Wao hukazana kutafuta wengine wa kulaumu isipokuwa wao. Wanakuwa na ushahidi kabisa wa jinsi wengine wamehusika kwenye yale wanayopitia. Lakini hata wanapomaliza hilo, bado mengine yanaibuka. Hayakomi kwa sababu mtu anakimbilia (more…)

2629; Hawataki ushauri wako.

By | March 13, 2022

2629; Hawataki ushauri wako. Nimewahi kuandika mara kadhaa kuhusu ushauri wa bure. Nikisisitiza usimpe mtu ushauri kama hajakuomba na usipokee ushauri kwa mtu kama hujamuomba akushauri. Pia nikaeleza jinsi ushauri wa bure ulivyo na gharama pale unapoufanyia kazi, kwa sababu unakuwa haujatolewa kulingana na uhitaji uliopo. Leo nakwenda kukupa sababu (more…)

2628; Ndiyo biashara yenyewe.

By | March 12, 2022

2628; Ndiyo biashara yenyewe. Sisi binadamu huwa tunafanya vitu kwa misukumo ya hisia mbili; tamaa na hofu. Huwa tunafanya kitu kama kuna kitu kizuri tunapata (tamaa) au kama hatutaki kupoteza tulichonacho (hofu). Kwa kujua hili, inakusaidia sana kuelewa kwa nini baadhi ya watu huwa wanafanya vitu ambavyo hukutegemea wafanye. Unaweza (more…)

2625; Usife.

By | March 9, 2022

2625; Usife. Katika safari ya mafanikio ya mtu yeyote yule, bahati ina mchango wake. Kila historia ya aliyefanikiwa, kuna mahali alikutana na bahati au fursa ya kipekee na ikampa manufaa makubwa. Kinachowatofautisha wanaokutana na bahati na ambao hawakutani nazo siyo bahati yenyewe, bali muda. Yaani siyo kwamba kuna watu wana (more…)

2624; Kanuni ya heshima au imani.

By | March 8, 2022

2624; Kanuni ya heshima au imani. Watu wamekuwa wanalalamika kwamba hawaheshimiwi au hawaaminiwi. Lakini ukiangalia kwa uhalisia, tatizo huanzia kwa watu kutokujiheshimu au kujiamini wenyewe. Leo napendekeza kanuni rahisi ambayo ukiifuata utajijengea heshima kubwa na kuaminika na wengine. Kanuni hiyo inakwenda hivi; Heshima/imani = utekelezaji/ahadi Ili heshima au imani iwe (more…)

2623; Gharama zilipojificha.

By | March 7, 2022

2623; Gharama zilipojificha. Kipo kichekesho kinaeleza mgahawa ambao ulitumia mbinu ya masoko kuwashawishi wateja kununua kwa wingi. Mgahawa huo uliweka tangazo kwa nje likieleza; kula leo watalipa wajukuu wako. Watu walivutiwa na hilo na kuingia kuagiza chakula. Baada ya kula wahudumu waliwaletea bili. Hapo ndipo wateja wakawa wanagoma kwamba tangazo (more…)

2622; Sababu zipo tayari.

By | March 6, 2022

2622; Sababu zipo tayari. Kama unataka kufanya kitu, au hutaki kukifanya, sababu zipo tayari. Kama utafanikiwa au utashindwa, sababu zipo tayari. Yaani sababu tayari ziko mbele yako, ni wewe tu uchague unataka nini, halafu uchukue sababu zinazoendana na kile unachotaka. Kama unataka kweli kupata kitu, sababu za kukitaka tayari unazo. (more…)

2621; Machache kuhusu wewe yanawatosha.

By | March 5, 2022

2621; Machache kuhusu wewe yanawatosha. Sisi binadamu tuna kasumba moja, kadiri tunavyokijua zaidi kitu ndivyo tunavyokichukulia kawaida na kukidharau. Lakini pale tunapokuwa hatukijui sana kitu huwa tunakiheshimu na kukichukulia kwa uzito mkubwa. Kwa kujua hili, wawekee watu mipaka ya kujua kuhusu mambo yako. Kadiri watu wanavyojua machache kuhusu maisha yako (more…)