Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (53/366); Fyonza Nguvu Yenye Kusudi.

By | December 23, 2021

#SheriaYaLeo (53/366); Fyonza Nguvu Yenye Kusudi. Katika safari yako ya kufikia ubobezi wa hali ya juu na mafanikio makubwa, unapaswa kuzungukwa na watu wenye nguvu ya kusudi na wanaopambana kufikia makubwa pia. Watu unaojihusisha nao, wanavyonza nguvu yako na wewe unafyonza nguvu yao pia. Kama utazungukwa na watu waliokata tamaa (more…)

#SheriaYaLeo (52/366); Tengeneza Kuhitajika.

By | December 22, 2021

#SheriaYaLeo (52/366); Tengeneza Kuhitajika. Wakati unajijengea ubobezi wako, tengeneza kuhitajika kwako na watu wengine. Wafanye wale unaowalenga kwenye kile unachofanya wakutegemee wewe zaidi. Hakikisha bila uwepo wako kuna mambo muhimu wanakosa au vitu vyao muhimu vinakwama. Hili ni muhimu sana kwa sababu kadiri unavyobobea ndivyo unavyozidi kutoza gharama kubwa kwenye (more…)

#SheriaYaLeo (51/366); Elewa jinsi ubongo unavyofanya kazi.

By | December 21, 2021

#SheriaYaLeo (51/366); Elewa jinsi ubongo unavyofanya kazi. Huwa tunadhani tunaweza kuruka hatua, kuepuka mchakato, kutumia kanuni rahisi au vipaji vyetu kufikia ubobezi kwa muda mfupi bila kuweka kazi. Ujio wa teknolojia umetufanya tuone kuna namna tunaweza kuukwepa mchakato mzima wa ubobezi. Kwa sababu teknolojia zimerahisisha mengi, tunadhani zinaweza pia kurahisisha (more…)

#SheriaYaLeo (50/366); Chagua muda.

By | December 20, 2021

#SheriaYaLeo (50/366); Chagua muda. Chochote unachochagua kubobea, unahitaji muda wa kutosha kuweka juhudi ili kuweza kupata matokeo makubwa. Kama una majukumu mengine mengi yanayochukua muda wako mwingi na kukuchosha, itakuwa vigumu kwako kifikia ubobezi unaotaka. Kile unachotaka kubobea kinapaswa kuwa ndiyo kipaumbele kikubwa kwako, hivyo kitengee muda wa kutosha. Yarahisishe (more…)

#SheriaYaLeo (49/366); Aina mbili za kushindwa.

By | December 19, 2021

#SheriaYaLeo (49/366); Aina mbili za kushindwa. Kuna aina mbili za kushindwa. Aina ya kwanza ni kushindwa kabla hata ya kuanza. Hapa unahofia kufanya kwa sababu unaona utashindwa au kwa sababu unaona bado muda haujawa sahihi, hujawa na maandalizi ya kutosha. Kwenye aina hii ya kushindwa hakuna chochote unachojifunza. Woga wako (more…)

#SheriaYaLeo (48/366); Ukweli Unaouma.

By | December 18, 2021

#SheriaYaLeo (48/366); Ukweli Unaouma. Hakuna njia ya mkato ya kufika kwenye ubobezi. Hakuna namna unaweza kukwepa mafunzo na ufanyaji wa kina wa kile unachotaka kubobea. Hayo yanahitaji muda ambao hauwezi kuharakishwa kwa namna yoyote ile. Kwa wastani, inachukua angalau miaka 10 ya kujifunza na kufanya kwa kina ndiyo mtu aweze (more…)

#SheriaYaLeo (47/366); Jifunze na kufanya kwa

By | December 17, 2021

#SheriaYaLeo (47/366); Jifunze na kufanya kwa kina. Watu wengi huwa wanajifunza na kufanya vitu kwa juu juu. Huwa wanataka yale maeneo ya kufurahisha na kusisimua. Lakini hivyo sivyo ubobezi unavyojengwa. Ubobezi unajengwa kwa kujifunza na kufanya kwa kina. Kujifunza na kufanya kwa kurudia rudia yale ya kawaida na yanayochosha. Hayo (more…)

#SheriaYaLeo (46/366); Umakini kwenye kujifunza

By | December 16, 2021

#SheriaYaLeo (46/366); Umakini kwenye kujifunza haujawahi kushindwa. Japo inaweza kuonekana inachukua muda mrefu kwenye kujifunza mpaka kufikia ubobezi wa hali ya juu, umakini, juhudi na muda unaowekwa kwenye kujifunza haupotei. Tafiti zilizofanywa kwenye eneo la ubobezi zinaonyesha kwamba mtu anahitaji kujifunza na kufanya kwa umakini mkubwa kwa angalau masaa elfu (more…)

#SheriaYaLeo (45/366); Ufuate Ukinzani.

By | December 15, 2021

#SheriaYaLeo (45/366); Ufuate Ukinzani. Sisi binadamu huwa tuna tabia ya kukimbia mambo ambayo ni magumu na yenye maumivu. Tunapenda kufanya yale ambayo ni rahisi kwetu na yasiyoonyesha udhaifu wetu. Kwa njia hii, tunashindwa kujijengea ubobezi, kwa sababu tunakuwa tumeweka nguvu na umakini wetu kwenye maeneo machache na ambayo ni rahisi (more…)

#SheriaYaLeo (44/366); Jinsi ya kujifunza haraka na kwa kina.

By | December 14, 2021

#SheriaYaLeo (44/366); Jinsi ya kujifunza haraka na kwa kina. Unapoingia kwenye mazingira yoyote mapya, wajibu wako ni kujifunza mambo mengi iwezekanavyo. Ili kufanikisha hilo, unapaswa kurudi kwenye hali ya utoto, kwa kuona kwamba watu wengine wanajua kuliko wewe na unategemea kujifunza kwao ili na wewe uweze kubobea. Unapaswa kuweka pembeni (more…)