2132; Nguvu Mara Mbili, Matokeo Sifuri…

By | November 1, 2020

Kwenye fizikia kazi inakuwa imefanyika pale nguvu zinapotumika kusogeza kitu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa maana hii, ukisukuma ukuta kama haujaanguka hakuna kazi umefanya, hata kama umetokwa jasho na kuchoka kiasi gani, kwa sababu nguvu uliyoweka haijasogeza ukuta huo kwa namna yoyote ile. Unaweza kuwa uliisikia dhana hii na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAMASA NA KIPAJI PEKEE HAVITOSHI…

By | November 1, 2020

“As habit is more dependable than inspiration, continued learning is more dependable than talent.” — Octavia Butler Ili kuanza kufanya kitu, unahitaji kuwa na hamasa ndani yako ya kukifanya. Lakini hamasa huwa haidumu, ni kitu cha muda mfupi tu. Hivyo ili uendelee kufanya, unapaswa kujijengea tabia, ikishakuwa tabia, inakuwa rahisi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISEME, ONESHA…

By | October 31, 2020

“Don’t talk about your philosophy, embody it.” – Epictetus Kusema ni rahisi na matendo ni magumu. Huwa tunapenda kusema kuliko kutenda. Lakini matendo yana sauti kubwa kuliko maneno. Hivyo kama unataka kueleweka na wengine, usiwe tu mtu wa kusema kwa maneno, badala yake onesha kwa vitendo. Chochote unachosimamia kwenye maisha (more…)

2130; Uimara Wa Madhaifu Yako…

By | October 30, 2020

Kila mtu ana madhaifu yake, lakini siyo wote ambao wanayajua madhaifu waliyonayo, kwa sababu wengi hawajapata nafasi ya kujitambua vizuri wao wenyewe. Kwa wale wanaoyajua madhaifu yao hilo limekuwa haliwasaidii, kwa sababu huchukua hatua moja kati ya hizi; Hujaribu kuyaficha madhaifu hayo kwa sababu hawataki yaonekane na wengine na kutumiwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UMASIKINI NA UTAJIRI…

By | October 30, 2020

“If you shape your life according to nature, you will never be poor. If you shape your life according to people’s opinions, you will never be rich.” – Epicurus Ukiyaendesha maisha yako kulingana na asili, kamwe huwezi kuwa masikini. Kwa sababu asili inataka mambo machache sana na ambayo yako ndani (more…)

2129; Kuhusu Maisha Kwenda Kama Unavyotaka…

By | October 29, 2020

Kuna kitu kimoja muhimu sana unachopaswa kuelewa kwenye safari ya maisha na mafanikio. Unaweza kupata kile unachotaka au kufika kule unakotaka kufika, lakini maisha hayataenda kama unavyotaka wewe yaende. Kupata unachotaka na maisha kwenda vile unavyotaka wewe ni vitu viwili tofauti kabisa. Na kutokujua tofauti hiyo kumekuwa kikwazo kwa wengi (more…)

2128; Hamsini Kwa Hamsini…

By | October 28, 2020

Umekuwa unasikia takwimu mbalimbali za nafasi ya mtu kufanikiwa. Watu kwenye jamii wamegawanywa kwenye makundi makubwa mawili, asilimia 1 ambao wamefanikiwa sana na asilimia 99 ambao hawajafanikiwa. Takwimu hizo ni za kweli pale unapoiangalia jamii na zinaleta picha ambayo inafanana kwenye maeneo mengi. Lakini kwako wewe, takwimu na nafasi hizo (more…)