2404; Nyenzo Muhimu Za Kujijengea Kwenye

By | July 31, 2021

2404; Nyenzo Muhimu Za Kujijengea Kwenye Maisha… Ni Mwanasayansi Archimedes aliyesema nipe mtarimbo mrefu na mahali pa kuuegemeza na nitaweza kuisogeza dunia. Alisema hayo kwa kujua nguvu ya nyezo, ambapo nguvu kidogo inaweza kuleta matokeo makubwa mno. Unatumia nyenzo kwenye shughuli zako za kawaida. Kung’oa msumari kwenye mbao siyo rahisi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NGUVU HAIPOTEI…

By | July 31, 2021

Kanuni ya fizikia inasema nguvu haitengenezwi wala haipotei, bali inabadilishwa kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine. Unapokuwa na hisia kali, huwa zinachochea nguvu kubwa ndani yako, nguvu hiyo huwa haiishi yenyewe. Nguvu hiyo hukimbilia kuleta uharibifu kama haitatumika vizuri. Hivyo panga kabisa mambo utakayofanya pale hisia zinapoibua nguvu ndani yako ili (more…)

2403; Itumie hiyo nguvu isikuumize…

By | July 30, 2021

2403; Itumie hiyo nguvu isikuumize… Kipindi cha nyuma kidogo huko Moshi kilianzishwa kiwanda cha pombe iliyoitwa Banana. Ni pombe kali iliyotengenezwa na ndizi. Ilikuwa mwenye duka anapoenda kununua, mpaka anafikisha dukani, kwenye kreti chumba mbili mpaka tatu zinapasuka zenyewe. Wakati wa kufungua pombe hiyo ilipaswa kufanywa taratibu la sivyo ilimwagika (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MTU PEKEE UNAYEWEZA KUMRIDHISHA…

By | July 30, 2021

Kuna mtu mmoja tu unayeweza kumridhisha na kumfurahisha kwenye maisha yako. Mtu huyo ni wewe mwenyewe. Utajiridhisha kwa kuishi maisha ya kweli kwako na siyo kuishi maisha ya maigizo ili kuwaridhisha wengine. Haijalishi unafanya nini, wapo watu watakaokuona wewe ni takataka na hufai kabisa. Siyo kwa sababu yako, bali kwa (more…)

2402; Kuna watu watakuona takataka…

By | July 29, 2021

2402; Kuna watu watakuona takataka… Kitu kimoja muhimu sana unachopaswa kukijua kwenye safari yako ya mafanikio, na ambacho kitapunguza sana makali ya safari hiyo kwako ni hiki; haijalishi unafanya nini, kuna watu watakuona wewe ni takataka kabisa. Wataona ni mtu usiyefaa na dunia ingekuwa bora kama usingekuwepo kabisa. Kwa kuwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI HISIA…

By | July 29, 2021

Hisia zako ndizo zinahusika kwenye maamuzi yote unayofanya. Unaweza kujiambia umetumia fikra, lakini ulichofanya kwenye fikra ni kuzihalalisha hisia zako. Bila hisia ni vigumu sana kufikia maamuzi yoyote yale, maana utatumia muda mwingi kuchambua kila chaguo kililopo. Lakini kwa hisia utachagua kile unachopenda kisha kuhalalisha kwa fikra kwamba ndiyo maamuzi (more…)

2401; Hisia, Hadithi, Mantiki…

By | July 28, 2021

2401; Hisia, Hadithi, Mantiki… Hivyo ni vitu vitatu tunavyotumia katika kufanya maamuzi yote kwenye maisha yetu. Huwa tunadhani tunafanya maamuzi kwa mantiki, kisha kuyajengea hadithi na kuwa na hisia nayo. Lakini sivyo tunavyofanya. Huwa tunafanya maamuzi kwa hisia kwanza, kisha tunatengeneza hadithi inayotetea maamuzi hayo na mwisho ndiyo tunatafuta mantiki (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UGUMU WA MABADILIKO…

By | July 28, 2021

Kama unataka kubadili matunda ambayo mtu unazalisha, kukata matawi hakutasaidia. Unapaswa kung’oa kabisa shina la mtu huo na kupanda mti mwingine. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mabadiliko ya maisha yetu. Hutaweza kuyabadili maisha kwa kuhangaika na tabia pekee, bali anza kwa kubadili imani ya ndani yako. Tabia ulizonazo ni matokeo (more…)