2091; Jiwekee Ukomo Wa Matumizi Ya Muda Wako…

By | September 21, 2020

Kinachotufanya tuahirishe yale tunayopanga kufanya, ni kwa sababu tuna machaguo mengi ya nini tunaweza kufanya na muda tulionao. Hivyo kile tulichopanga kufanya kinapoonekana kigumu au chenye changamoto, ni rahisi kukimbilia kwenye kingine kinachoonekana rahisi zaidi. Kwa njia hii, unajikuta ukitoroka yale uliyopanga kufanya, ukijipa sababu nyingi unazoweza kuona ni za (more…)

2090; Angalia Umri Wako Usiwe Kikwazo Kwako…

By | September 20, 2020

Moja ya vikwazo ambavyo vimekuwa vinawazuia watu kufanikiwa lakini hawavijui ni umri. Wengi hawajawahi kukaa chini na kutafakari jinsi umri unaathiri hatua wanazochukua, wanadhani wanachofanya ndiyo wanachotaka, kumbe umri wao umekuwa na ushawishi. Kwa vijana, wengi huwa hawaridhiki na kile walichonacho, wanapenda mabadiliko ya haraka, wapo tayari kujaribu vitu vipya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKIONA NI RAHISI, PATA WASIWASI…

By | September 20, 2020

“Bad things are easy to do, good things are done only with work and effort.” — Dhammapada Matapeli wana siri moja ya kuwanasa watu wanaotaka kuwatapeli. Huwa wanafanya kitu kionekane kuwa rahisi kabisa kufanya. Na kwa kuwa watu wanapenda urahisi, basi hunasa kwenye mitego hiyo na kutapeliwa. Vitu vibaya na (more…)

2089; Unasikiliza Watu Wa Aina Gani?

By | September 19, 2020

Hatua unazopiga na matokeo unayopata, vinategemea sana aina ya watu waliokuzunguka. Watu hao wanagawanyika kwenye makundi mawili na ndani ya kila kundi wanagawanyika mara mbili. Kundi la kwanza ni wale wanaokutia moyo na kukushauri upige hatua zaidi. Hawa wanakubaliana na kile unachofanya na wanakupa sababu ya kuendelea. Ni rahisi kuwapenda (more…)

2088; Hasira Zako Haziwezi Kubadili Kanuni Za Asili…

By | September 18, 2020

Umeamka asubuhi, unataka kuwahi mahali, unajua kabisa usafiri wako uko vizuri, ila asubuhi hiyo unajaribu kuuwasha na hauwaki. Ulishapanga kabisa muda uliozoea kufika eneo husika na sasa usafiri ambao umekuwa unatumia kila siku hauwaki. Unaweza kupata hasira, ukakazana kuendelea kuwasha ukitegemea uwake kwa haraka kama ulivyo na haraka wewe, lakini (more…)