UKURASA WA 1259; Upo Kwenye Upande Upi Wa Huu Mchezo Muhimu…

By | June 12, 2018

Maisha ni mchezo, najua unajua hilo, ila kukumbushana ni muhimu. Kila mchezo una sheria zake, ni muhimu kuzijua kabla hujaendelea na mchezo. Maana kuvunja sheria, hata kama  huzijui unapata adhabu kubwa. Sasa kuna hili muhimu sana kuhusu mchezo huu wa maisha, ambalo ni upande upi wa mchezo ambao umechagua kucheza. (more…)

UKURASA WA 1258; Unapokosea Kwenye Kuwaelewa Wengine…

By | June 11, 2018

Umewahi kujiambia kwamba watu hawaeleweki? Kwamba ulitegemea wafanye kitu fulani halafu wao wakafanya kitu kingine tofauti kabisa? Ukweli ni kwamba siyo watu hawaeleweki, ila wewe ndiyo huelewi jinsi ya kuwaelewa watu. Kosa kubwa tunalofanya kwenye kuwaelewa wengine ni kujitumia sisi wenyewe kama kipimo cha kuwaelewa wengine. Kwamba kwa sababu sisi (more…)

UKURASA WA 1257; Jiwekee Karantini Kwenye Maeneo Haya Muhimu Ya Maisha Yako…

By | June 10, 2018

Yapo magonjwa ya kuambukizwa, ambayo ni hatari sana, ambayo yanasambaa kwa kasi na kuua wengi. Njia pekee ya kukabiliana na magonjwa ya aina hii huwa ni kuweka karantini wagonjwa au wasio wagonjwa. Unaondoka kila namna ya ugonjwa kuweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Yapo maeneo ya (more…)

UKURASA WA 1256; Maumivu Ni Sehemu Ya Mchezo…

By | June 9, 2018

Maisha ni mchezo, na ili ufanikiwe kwenye mchezo wowote ule, lazima kwanza uzijue sheria za mchezo, ujue yapi unapaswa kufanya, yapi hupaswi kufanya, na yapi unategemea kupata. Moja ya sheria zisizosemwa za kila mchezo ni maumivu, kila mchezo una aina fulani ya maumivu. Ambapo mchezaji yeyote anayeshiriki mchezo huo, anajua (more…)

UKURASA WA 1255; Makundi Makubwa Mawili Ya Watu Duniani…

By | June 8, 2018

Kuna makundi makuu mawili ya watu, ambapo watu wote wanaingia kwenye kundi moja au jingine. Kundi la kwanza ni watu jasiri, watu ambao wapo tayari kuchukua hatua na kupata kile ambacho wanakitaka. Hawa ni watu ambao kwa nje wanaonekana kama hakuna wanachohofia, wapo tayari kuchukua hatua na wanapata kila wanachokitaka. (more…)

UKURASA WA 1254; Sheria Nyingine Tatu Muhimu Kwenye Mafanikio…

By | June 7, 2018

Aah kocha usiniambie kuna sheria nyingine tena ambazo bado sijazijua… Ni kweli kuna sheria nyingine za mafanikio, lakini si kweli kwamba hujazijua, ni sheria zile zile ambacho tumekuwa tunashirikishana mara kwa mara, ila zimeelezewa kwa namna tofauti. Najua wengi hatupendi sheria, lakini bila ya sheria, za kujiwekea sisi wenyewe au (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FANYA MAJARIBIO MENGI ZAIDI…

By | June 7, 2018

“All life is an experiment. The more experiments you make, the better.” — Ralph Waldo Emerson Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA (more…)

UKURASA WA 1253; Kwa Nini Hatua Unazochukua Hazitakupa Mafanikio…

By | June 6, 2018

Watu wanasema kama kufanya kazi kwa nguvu na juhudi kungekuwa ni ufunguo wa mafanikio, basi punda wangekuwa na mafanikio makubwa sana. Ni kweli kwa asili, punda anabeba mizigo mizito sana na anaweza kustahimili mazingira magumu sana kama ya ukame. Lakini siyo mnyama mwenye mafanikio makubwa. Kwa upande wa pili, simba (more…)