Mbinu za kisaikolijia za kistoa – KUTAFAKARI/TAHAJUDI.

By | April 9, 2017

  Mwanafalsafa Seneca anatukumbusha kwamba kila siku tunahitaji kupata muda wa kutafakari kuhusu maisha yetu na kile tulichofanya siku nzima. Mwisho wa siku, tunahitaji kupata muda wa kujiuliza siku yetu imekwendaje na yale tuliyofanya tumefanyaje. Ni yapi ambayo tumefanya vizuri, Yapi ambayo tumekosea na Yapi ambayo tunaweza kuboresha zaidi. Epictetus (more…)

Mbinu za kisaikolijia za kistoa – KUJINYIMA MWENYEWE.

By | April 9, 2017

Moja ya mizigo mikubwa ambayo watu wanajijengea wenyewe ni tamaa na kupenda raha. Hivyo watu wengi hukazana sana kuhakikisha kwamba wanapata kila raha wanayotaka. Lakini mtego unakuja, pale wanapopata raha hiyo, wanakiwa na hofu ya kuipoteza na hivyo wanashindwa kuifurahia raha waliyopata. Wastoa wanatushirikisha mbinu mbili muhimu za kuweza kuondokana (more…)

Fatalism; kuishi kama asili ilivyopanga.

By | April 9, 2017

Watu wengi wa enzi za roma, watu waliamini ya kwamba, hatima ya mtu imeshapangwa. Yaani hata ufanye nini, hakuna namna unavyoweza kubadili hatima ya maisha yako. Na hii ilipelekea wengi kutokuhamasika kuchukua hatua kubwa kwenye maisha yao. Lakini wastoa walijua namna bora ya kutumia hilo, badala tu ya kukubali na (more…)

Utatu wa udhibiti.

By | April 9, 2017

  Wastoa wanaelewa kwamba hawawezi kudhibiti kila kitu kinachotokea kwenye maisha yao. Na kwa vile mambo mengi yanayotokea yanatuathiri moja kwa moja, yana mchango kwenye furaha yetu kwenye maisha. Hivyo ili kuwa na maisha yenye furaha na yasiyoingiliwa na yale yanayoendelea, wanafalsafa wa ustoa walishauri tuyagawe mambo yanayotokea kwenye makundi (more…)

UKURASA WA 830; Kirusi Kinachoua Ndoto Za Wengi Kwa Haraka…

By | April 9, 2017

Magonjwa yanayosababishwa na vizuri ni magonjwa ambayo huwa yana changamoto sana kwa sababu vizuri huwa wanasambaa haraka na pia ni wagumu kutibika. Hii ni kwa sababu vizuri wanaweza kuwa kama viumbe hai na wakati mwingine wakawa kama siyo viumbe hai, yaani wakawa kama jiwe tu. Dawa zinazotengenezwa kuua, zina uwezo (more…)

UKURASA WA 829; Tofauti Ya Wengi Na Sisi Katika Utajiri…

By | April 8, 2017

Watu wengi wanatafuta utajiri, lakini sisi wanamafanikio tunatafuta zaidi ya utajiri. Wengi wanafikiri wakishapata utajiri basi wamemaliza kila kitu, lakini sisi wanamafanikio tunajua utajiri ni sehemu ndogo ya maisha, tunahitaji mafanikio kwenye maeneo mengine mengi ya maisha yetu ili kuwa na maisha bora na yenye furaha. Wengi wanabeza utajiri, hasa (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UTAMU NA UCHUNGU….

By | April 7, 2017

Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo. Tumepata nafasi ya kipekee leo kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora kabisa. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu UTAMU NA UCHUNGU… Utamu (more…)

UKURASA WA 828; Hakuna Mkono Wa Mtu….

By | April 7, 2017

Mara nyingi kuna vitu ambavyo tunavitaka, tunakazana sana kuweka juhudi ili kuvipata, na tunaona kila dalili kwamba tunakwenda kuvipata, ila ghafla mambo yanabadilika na tunakosa tulichotaka. Pamoja na juhudi zote tulizoweka, pamoja na kufanya kila tulichopaswa kufanya, lakini tunashindwa kupata tulichotaka. Ni rahisi kwenye nyakati kama hizi kufikiri kwamba kuna (more…)