💥 #TAFAKARI YA LEO; STATUS QUO…

By | November 25, 2016

Hongera rafiki yangu kww nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweks juhudi zaidi kwenye kile tulichochagua kufanya ilo tuweze kupata matokeo bora zaidi. Rafiki, tutumie muda wa leo vizuri, maana ukishapita hatuwezi kuupata tena kwenye maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu STATUS QUO….. (more…)

UKURASA WA 695; Tumia Nafasi Yako Ya Kuchagua Vizuri…

By | November 25, 2016

Kwenye maisha yetu, tunazo nafasi za kuchagua vile tunavyotaka wenyewe na nafasi nyingine hatuwezi kuchagua wenyewe, tunajikuta tayari tupo kwenye nafasi hizo. Kwa mfano huwezi kuchagua uzaliwe na wazazi gani, au wadogo na ndugu zako wawe watu wa aina gani. Hawa ni watu wanaokuja na kuwepo kwenye maisha yako bila (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; BORA UPOTEE…

By | November 24, 2016

Habari za asubuhi ya leo rafiki? Ni siku nyingine mzuri sana ambayo tumeianza. Ni ile siku ambayo kuna mambo ulijiambia nitafanya kesho. Nataka nikukumbushe tu rafiki yangu kwamba kesho yenyewe ndiyo imeshafika sasa. Usipeleke tena kwenye kesho nyingine zaidi ya leo. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUPOTEA, kuliko kubaki hapo (more…)

UKURASA WA 694; Miliki Chochote Unachofanya…

By | November 24, 2016

Katika maisha, kuna makundi mawili makubwa ya watu; Kuna wamiliki wa vitu, hawa ni wale ambao wanachukua mamlaka makubwa juu ya kitu chochote na kuhakikisha kinakwenda kama wanavyotaka kiende. Watu hawa wanaweka juhudi kubwa kuhakikisha wanatoa matokeo makubwa. Kama kitu chochote hakitokei, wanajua ni kwa sababu kuna juhudi hawajaweka. Kuna (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; NI MIMI MWENYEWE….

By | November 23, 2016

Leo ni siku bora na ya kipekee sana kwetu, Ni siku ambayo tumekuwa tunaisubiri ili kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yetu. Tusiahirishe tena yale tuliyopanga leo, kwa sababu hayuwezi kupata siku bora kama hii tuliyopata leo. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MIMI MWENYEWE… Nipo hapa nilipo sasa kwa sababu MIMI (more…)

UKURASA WA 693; Akili Yako Imepitwa Na Wakati…

By | November 23, 2016

Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta kwa muwa mrefu lazima utakuwa unajua kwamba programu za kompyuta kuna wakati huwa zinakuwa zimepitwa na wakati. Kwa neno la kingereza wanasema OUTDATED. Angalia mfano programu kuu ya kuendesha kompyuta inayoitwa windows, zimekuwepo nyingi na zote zinapitwa na wakati na hivyo kuja nyingine. Mfano (more…)

UKURASA WA 692; Tegemea Na Jipange Kwa Hili Kama Unataka Kufanikiwa….

By | November 22, 2016

Jambo kubwa linalowashangaza wengi wanaoianza safari ya mafanikio, ni namna watu ambao waliwategemea wawape moyo wanakuwa wa kwanza kuwavunja moyo na kuwakatisha tamaa. Watu ambao walikuwa wanakuambia unaweza kufanikiwa, unaweza kufanya makubwa na kauli nyingine kama hizo, wanapokuona unaanza kufanya wanakuwa wa kwanza kukuambia unakosea, au huwezi au utashindwa. Hii (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; HUJACHELEWA….

By | November 21, 2016

Habari rafiki yangu? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Tutumie muda wetu wa leo vizuri rafiki, kwa sababu hatutakuja kuupata tena. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUCHELEWA…. Kwenye maisha kuna wakati unajiona kama umechelewa. (more…)

UKURASA WA 691; Imani Inayowatenganisha Watu Na Utajiri…

By | November 21, 2016

Kuna imani ambazo zinakaribisha fedha na hivyo kuleta utajiri na pia kuna imani ambazo zinafukuza kabisa fedha. Ndani ya jamii zetu, imani kubwa zilizotawala ni zile za kufukuza fedha. Moja ya imani ambayo inafukuza fedha na kuwafanya wengi kubaki kwenye umasikini ni imani ya UHABA. Jamii na watu wanaokuzunguka wanakufanya (more…)