Tag Archives: FIKRA MBADALA

Waliofika kileleni…

By | December 10, 2014

Watu waliofika kwenye kilele kikubwa sio kwa sababu watu hao waliruka na kujikuta kileleni, ila kwa sababu watu hao, wakati wenzao wamepumzika wao waliendelea kukomaa na kuendelea na safari. Endelea na safari yako wakati wengine wamelala… Endelea na safari yako wakati wengine wanastareheka… Endelea na safari yako wakati wengine wanabishana (more…)

Ana Miaka 53 Ila Bado Analishwa Uji…

By | December 9, 2014

Kwa kawaida mtu yeyote anayezaliwa huwa anapitia vipindi tofauti kwenye maisha yake. Kwanza kabisa anaanza kama mtoto ng’aa, ambapo anakuwa anategemea kunyonya maziwa ya mama tu. Anaendelea kukua na baadae anakuwa analishwa uji, huku akikazana kutambaa na hatimaye kutembea. Baada ya muda anaanza kula matonge ya ugali na kukimbia mwenyewe.. (more…)

Nyasi Za Upande Wa Pili Ni Za Kijani Zaidi…

By | December 8, 2014

Angalia zile nyasi za upande wa pili, ni za kijani zaidi ya nyasi zilizopo upande wako… Hii ni fikra ambayo huwa inamjia kila mtu katika sehemu aliyopo iwe ni maisha, kazi au biashara. Unaweza kuona wenzako wana maisha mazuri kuliko hayo uliyoko nayo kwa sababu tu unaona wanatembelea magari mazuri (more…)

Tulikuona Wakati Unakuja Mjini…

By | December 7, 2014

Tulikuona wakati unakuja mjini, usijione mjanja leo… Ulikuja umevaa yeboyebo na nguo umebeba kwenye mfuko wa rambo, leo unajiona unajua sana… Hayo ni maneno ya hovyo sana yanayotolewa na watu walioshindwa. Watu ambao wamepoteza muda wao kwa kufikiri wao ni wakongwe na anakuja mtu na kuwaacha wakishangaa. Ili kujifariji kwamba (more…)

Bado Hujachelewa…

By | December 6, 2014

Kuna bwana mmoja alikuwa analalamika ni jinsi gani alikuwa anapenda kujifunza kupiga kinanda ila akakosa muda kwenye maisha yake. “Kwa nini usianze sasa” rafiki yake alimuuliza. “Unashangaza wewe” yule bwana alimjibu. “Nina miaka hamsini sasa, nikianza kujifunza leo itanichukua miaka mitano mpaka nijue kupiga kinanda vizuri, wakati huo nitakuwa na (more…)

Tunarudia Makosa Yale Yale…

By | December 6, 2014

Hakuna makosa mapya, tunarudia makosa yale yale. Ila kwa kuwa teknolojia imekua basi na kiwango chetu cha kufanya makosa yale yale tuliyokuwa tunayafanya zamani kimebadilika. Watu wamekuwa wakiambiwa wasiue zaidi ya miaka 4000 iliyopita sasa, lakini mpaka leo bado wanaua. Usiibe, usizini, bado kila siku tunarudia makosa haya haya. Hii (more…)

Mwalimu Anakusubiri, Chukua Hatua Sasa…

By | December 5, 2014

Mwanafunzi anapokuwa tayari mwalimu hutokea… Huu ni usemi wa kale kidogo ila unaobeba maana kubwa sana. Mwanafunzi anapokuwa tayari mwalimu hutokea, sio kwa sababu mwalimu alikuwa anasubiri mwanafunzi awe tayari ndio ajitokeze bali mwalimu alikuwepo muda wote ila mwananfunzi anapokuwa tayari ndio anamuona mwalimu kuwa yupo. Mambo mengi kwenye maisha (more…)

Hii Ndio Ardhi Yenye Utajiri Mkubwa Sana Duniani.

By | December 4, 2014

Kuna ardhi yenye utajiri na thamani kubwa sana duniani… Ardhi hiyo sio yenye visima vya mafuta.. Na wala sio ardhi yenye migodi ya madini… Bali ardhi hiyo ni makaburi, Makaburi yamejaa ndoto nyingi sana ambazo hazikutimizwa. Kuna mawazo makubwa ya kibiashara ambayo hayakutimizwa… Kuna mawazo na ndoto kubwa za mabadiliko (more…)