#TAFAKARI YA LEO; USHAURI WAKO NI MZURI KWAKO…

By | June 6, 2021

Unaweza kuona una ushauri mzuri sana kwa wengine, lakini tambua siyo wote watakaoona uzuri wa ushauri huo kama unavyouona wewe. Na hata kama watauona huo uzuri, bado siyo wote watakaofanyia kazi ushauri wako. Na kama unawashauri bila ya wao kuomba, ndiyo kabisa hawatajihangaisha na ushauri wako. Watu huwa hawathamini ushauri (more…)

2348; Kama hawajakuomba, usijisumbue…

By | June 5, 2021

2348; Kama hawajakuomba, usijisumbue… Moja ya kitu nimewahi kuandika na wengi wakauliza kwamba hawakuelewa ni hiki; usitoe ushauri kwa mtu ambaye hajakuomba, usipokee ushauri kwa mtu ambaye hujamuomba. Unaweza kuona kama watu wanahitaji sana ushauri wako, unaona kabisa wanakwenda kukosea na kwa kuwashauri utawasaidia wasiende kuanguka. Lakini unakumbuka umewahi kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAPATA UNACHOTAFUTA…

By | June 5, 2021

Kama unatafuta sababu za kutokufanya kitu, utazipata nyingi tu. Na kama unatafuta njia ya kufanya kitu, utazipata za kutosha. Akili yako ina uwezo mkubwa wa kuvuta kwako kile unachotaka. Hivyo kama hujapata unachotaka, hebu anza kwa kuangalia akili yako inatafuta nini zaidi na utagundua kila ulichonacho sasa ndiyo akili yako (more…)

2347; Muda sahihi wa kufanya kitu kikubwa…

By | June 4, 2021

2347; Muda sahihi wa kufanya kitu kikubwa… Haujawahi kuwepo, Hakuna wakati utakaosema uko tayari kufanya kitu ambacho ni kikubwa. Kila wakati utaona unahitajika kusubiri zaidi kwa sababu muda bado haujawa sahihi. Iwe ni kuanzisha biashara, kubadili kazi au kuanza mradi wowote mkubwa, utaona bado muda haujawa sahihi. Hupaswi kuruhusu hili (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIYAPOTEZE MAISHA KWA YASIYO NA TIJA…

By | June 4, 2021

Maisha tayari ni mafupi, mambo ya kufanya ni mengi na muda ulionao ni mchache. Usikubali kuyapoteza maisha yako kwa kuhangaika na mambo yasiyo na tija kwako kama kubishana. Usihangaike na kila anayekupinga au kuamini tofauti na wewe. Hata ukihangaika kuwabadili, bado hawatabadilika. Lakini kama jambo ni muhimu kweli, kama inabidi (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha ushonaji wa nguo.

By | June 3, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha ushonaji wa nguo. Ufundi wa kushona nguo huwa unaonekana ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujifunza na kufanya. Na hivyo wengi wamekuwa hawalipi uzito hilo, wale wanaofanya hubaki wakifanya kwa mazoea na kulalamika hawawezi kuingiza kipato kwa njia hiyo. Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza (more…)

2346; Kabla Hujabishana…

By | June 3, 2021

2346; Kabla Hujabishana… Wengi hupenda kubishana lakini ubishani wao huwa hauna manufaa yoyote kwao. Kwani huwa wanashindwa kuwashawishi wale wanaobishana nao. Huwa nashauri sana watu kuachana na ubishani wa aina yoyote ile. Lakini kuna nyakati ubishani haukwepeki, hasa pale unapotaka kusimamia kile kilicho sahihi. Lipo sharti moja muhimu unalopaswa kutimiza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIKUBALI MSONGO HUU…

By | June 3, 2021

Msongo wa mawazo unaosababishwa na matumizi ya mitandao ya kijamii ni wa kujitakia. Unajiweka mwenyewe kwenye mazingira ambayo watu wengi unaojihusisha nao huwajui halafu unakazana kujilinganisha nao wakati kila mmoja anaishi maisha ya maigizo huko mitandaoni. Unaweza kujionea mwenyewe kwa nini lazima upate msongo kwenye mitandao hiyo usipokuwa makini. Ni (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia pikipiki.

By | June 2, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia pikipiki. Kila mtu anapofikiria kuingiza kipato kwa pikipiki anafikiria njia moja iliyozoeleka ambayo ni bodaboda. Hilo limepelekea bodaboda kuwa nyingi mitaani na ushindani kuwa mkali. Kuna njia nyingine nyingi za kuingiza kipato kwa kutumia pikipiki. Hapa ni 10 katika njia hizo. Njia iliyo (more…)

2345; Mageuzi ya teknolojia yamepiku mageuzi ya akili…

By | June 2, 2021

2345; Mageuzi ya teknolojia yamepiku mageuzi ya akili… Tunachokiona kwenye maisha ya sasa, hasa zama hizi za mitandao ya kijamii, ni mageuzi ya teknolojia kwenda kasi kuliko mageuzi ya akili. Kwa mamilioni ya miaka, binadamu tulikuwa tunaishi kwenye makundi madogo madogo ya watu wasiozidi 30. Hiyo ilikuwa rahisi kumjua kila (more…)