#TAFAKARI YA LEO; HAITOSHI KUJUA, FANYA…

By | November 12, 2020

“It is not enough to know, we must also apply; it is not enough to will, we must also do.” – Johann Wolfgang von Goethe Kujua pekee haitoshi, ni lazima uweke kwenye matendo kile unachojua ndiyo uweze kunufaika nacho. Hekima ni kuweka kwenye matendo maarifa unayoyapata. Haijalishi unajua kiasi gani, (more…)

2142; Wakati Gani Wa Kuyaamini Machale…

By | November 11, 2020

Kuna wakati unafanya maamuzi bila ya kujua kwa nini unayafanya na yanaishia kuwa maamuzi sahihi. Hapo unajiambia kwamba machale yamekucheza na ukaona kitu ambacho huwezi kukielezea lakini ni sahihi. Lakini pia kuwa wakati machale hayo hayo yanakupoteza, yanapelekea ufanye maamuzi ambayo siyo sahihi na yanayokugharimu. Machale ni zile hisia unazozipata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UBAYA UNAJIFANYIA MWENYEWE…

By | November 11, 2020

“To do harm is to do yourself harm. To do an injustice is to do yourself an injustice — it degrades you.” — Marcus Aurelius Unapowafanyia wengine ubaya, siyo wao pekee wanaoathirika, bali wewe mwenyewe unaathirika zaidi. Huwezi kuwadanganya wengine kama hujajidanganya wewe mwenyewe. Unapowaumiza wengine, ni kwa sababu ndani (more…)

2141; Hakuna Kinachofanywa Mara Moja…

By | November 10, 2020

Simu ya Iphone iko kwenye toleo la 12, wakati toleo la kwanza linatoka, ilikuwa ni mapinduzi makubwa mno kwenye ulimwengu wa teknolojia na mawasiliano. Ilikuwa ni kitu ambacho hakijawahi kuonekana wala kudhaniwa na ilibadili kabisa maisha ya watu. Ingetosha kwa kampuni ya Apple kusema wamemaliza, wameweza kuleta mapinduzi makubwa na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MSIMAMO NI MGUMU…

By | November 10, 2020

“It’s easy to be great. It’s hard to be consistent.” – Steve Martin Kuna watu wengi ambao huwa wanafanikiwa kupiga hatua fulani, lakini baada ya hapo wanaanguka vibaya. Kufanikiwa siyo kitu kigumu sana, ila kubaki kwenye mafanikio hayo ndiyo kitu kigumu na kinachowashinda wengi. Kubaki kwenye mafanikio inamtaka mtu kuwa (more…)

2140; Siyo Kwa Mapenzi Yako…

By | November 9, 2020

Mwandishi mmoja amewahi kusema kadiri mtu unavyolazimisha kwamba maamuzi yako hayaathiriwi na hisia ndivyo maamuzi hayo yanavyokuwa na hisia. Wote tunajua kwamba sisi binadamu ni viumbe wa kihisia, maamuzi mengi tunayofanya ni kwa hisia kwanza na baadaye tunayahalalisha kwa kufikiri. Lakini tunapenda kujiaminisha kwamba tunafanya maamuzi yetu kwa kufikiri, kitu (more…)

2139; Usitumie Nguvu Kwenye Haya…

By | November 8, 2020

Kama unataka kulala, huwezi kutumia nguvu kutafuta usingizi. Ukiingia kitandani kwa kujiambia unakwenda kutafuta usingizi kwa nguvu, hutaupata kabisa. Lakini unapoingia kitandani ukiwa umejiachia kwamba unapumzika, usingizi unakuja wenyewe. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye furaha na mapenzi, huwezi kulazimisha, ukitumia nguvu ndivyo unavyozidi kupoteza vitu hivyo. Tukianza na furaha, kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ONGEA NA WAFU…

By | November 8, 2020

“To live the best life,” the Oracle told Zeno, “you should have conversations with the dead.” Kama unataka kuwa na maisha bora, unapaswa kuongea na wafu. Na hapa siyo kwa kufanya matambiko, bali kwa kusoma maarifa yaliyoachwa na wale waliotutangulia hapa duniani miaka mingi iliyopita. Wanafalsafa na waandishi mbalimbali waliweka (more…)