Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; FANYA CHOCHOTE…

By | January 12, 2021

Kama upo njia panda na hujui kipi cha kufanya, anza kufanya chochote. Kwa kufanya chochote ni rahisi kufika kwenye kilicho sahihi kwako kufanya kuliko kuendelea kusubiri. Kwa kuanza na chochote unajifunza na kupata msukuko wa kuendelea kuliko kusubiri. Unaweza kusubiri utakavyo, lakini tambua muda haukusubiri na muda ukishapita haurudi tena. (more…)

2203; Fanya Chochote Ili Kujua Cha Kufanya…

By | January 11, 2021

Kanuni za kisayansi, hasa kanuni za fizikia, ni kanuni ambazo zinatokana na asili. Hiyo ina maana kwamba kanuni hizo zinafanya kazi kila mahali na kwa kila hali. Moja ya kanuni hizo ni kuhusu mwendo, ambayo inasema kitu kilichosimama kitaendelea kusimama na kilicho kwenye mwendo kitaendelea na mwendo mpaka nguvu ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIPOST UJINGA, FANYA KAZI…

By | January 11, 2021

Mitandao ya kijamii imewageuza watu kuwa misukule wanaofanya kazi bila kulipwa. Inawahadaa watu kwa umaarufu feki unaopatikana kwa kupost vitu vya kijinga mtandaoni. Lakini umaarufu huo hauna manufaa kwa mtu zaidi ya kumharibia sifa yake. Umaarufu wenye manufaa ni ule unaotokana na kazi inayotoa thamani kwa wengine, ila huo unahitaji (more…)

2202; Umaarufu Feki Na Halisi…

By | January 10, 2021

Watu wengi wanapenda umaarufu, ila huwa hawajali ni umaarufu wa aina gani, una manufaa gani na changamoto zipi zinakuja na umaarufu. Umaarufu tunaweza kuugawa kwenye makundi mawili, feki na halisi. Umaarufu halisi ni ule unaotokana na ubobezi ambao mtu amefikia katika kile anachofanya, na ambacho kina manufaa makubwa kwa wengine. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA CHANYA KUNALIPA…

By | January 10, 2021

Katika kila jambo au hali unayopitia, kuwa chanya kunalipa kuliko kuwa hasi. Kuwa chanya kunakuonesha fursa zaidi wakati kuwa hasi kunakuonesha matatizo zaidi. Kuwa chanya kunakupa matumaini wakati kuwa hasi kunakukatisha tamaa. Pamoja na manufaa haya ya kuwa chanya, bado wengi hukimbilia kuwa hasi. Hiyo ni kwa sababu kuwa hasi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FANYA MAAMUZI YA MAISHA YAKO…

By | January 9, 2021

Watu wengi ni wazito kufanya maamuzi ya maisha yao. Hiyo ni kwa sababu kufanya maamuzi ni kugumu kuliko kufuata mkumbo. Wengi huishia kuangalia wengine wanafanya nini na kufanya pia, bila kujiuliza kama ndiyo kitu sahihi kwao kufanya. Wewe usiwe hivyo, usiruhusu maisha yako yaendeshwe na wengine kwa namna watakavyo. Fanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUIFANYA DUNIA IWE UNAVYOTAKA…

By | January 8, 2021

Hicho ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako kabisa. Lakini wengi wamekuwa wakihangaika nacho, wakitaka kuifanya dunia iende wanavyotaka wao na watu wawe vile wanavyotaka. Hilo linaposhindikana wanaumia na kukata tamaa. Mtu pekee unayeweza kumdhibiti na kumbadili hapa duniani ni wewe mwenyewe. Hivyo peleka nguvu zako kwenye kujibadili na (more…)

2199; Aina Mbili Za Ushauri…

By | January 7, 2021

Kuna aina mbili za ushauri, unazopaswa kuzijua na jinsi unavyoweza kutumia kwenye kile unachopitia. Aina ya kwanza ni ushauri wa wazi, huu ni ule ushauri unaotolewa kwa wazi na unaoweza kumlenga kila mtu. Mfano unaposoma makala yenye ushauri kuhusu biashara, kazi au fedha, inaweza kuwa na mambo mazuri, lakini mengi (more…)