Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

BIASHARA LEO; Mteja Wa Mfano Wa Biashara Yako…

By | August 7, 2018

Kosa moja wanalofanya wafanyabiashara wengi ni kuanzisha biashara zao kwa kujifikiria wao wenyewe, au kuangalia wafanyabiashara wengine wanafanya nini. Biashara yoyote inayoanzishwa na mtu kwa sababu anafikiria ananufaikaje na biashara hiyo pekee, au kwa kuwaangalia wengine wanaofanya biashara hiyo na kujiambia inalipa ndiyo maana wapo, lazima biashara hiyo ishindwe. Biashara (more…)

UKURASA WA 1315; Kwa Nini Ni Vigumu Sana Kuwa Wewe?

By | August 7, 2018

Kama kuna kitu kilipaswa kuwa rahisi kwenye maisha yetu, ni mtu kuwa wewe, kuwa kile ambacho umezaliwa na kuletwa hapa duniani kuwa. Kama ambavyo ukichukua yai la kuku na ukatamishia kwenye kanga, bado atatoka kuku, na hata kifaranga wa kuku atalelewa pamoja na vifaranga wa kanga, bado atabaki kuwa kuku. (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujawauzia Wengine Bidhaa Au Huduma Yako, Wauzie Hichi Muhimu…

By | August 6, 2018

Umewahi kukutana na mtu ambaye anaweza kuuza kitu chochote kwa mtu yeyote. Yaani unaenda mahali, unajiambia kabisa kwamba hutanunua, lakini unakutana na mtu, na kwa jinsi anavyokupokea, kwa jinsi anavyokusikiliza, jinsi anavyokuelezea unachouliza, unajisikia vibaya kutokununua? Kama umewahi kuwa kwenye hali kama hiyo, basi unajua kwamba ulinunua kitu siyo kwa (more…)

UKURASA WA 1314; Unaponasa Kwenye Yale Yasiyo Muhimu…

By | August 6, 2018

Moja ya sababu kubwa kwa nini kila mmoja wetu anapaswa kuwa na orodha ya vitu atakavyofanyia kazi kwenye siku yake ni kwamba siku inavyoharibika huwa siyo rahisi kuonekana. Unachoshangaa ni siku yako imeisha, umechoka, lakini ukiangalia, hakuna kikubwa umefanya, hakuna matokeo mazuri uliyozalisha. Tunazungukwa na kila aina ya usumbufu, na (more…)

BIASHARA LEO; Dawa Inayofanya Kazi Ni Inayouma…

By | August 5, 2018

Kuna tukio la kisaikolojia linatokea pale mteja anapotoa fedha yake aliyoipata kwa shida kukulipa kwa kile unachouza. Kwa sababu kwanza akishakupa fedha hiyo maana yake hawezi kuitumia kwa mambo mengine ambayo yanaweza kuwa muhimu kwake. Na pili, mteja anahitaji kupata uhakika kwamba anacholipia ni sahihi na moja ya kipimo anachotumia (more…)

UKURASA WA 1313; Siyo Mwonekano, Bali Matokeo…

By | August 5, 2018

Tunaishi kwenye dunia ambayo watu wanajali zaidi mwonekano wa nje kuliko matokeo ambayo wanatoa. Watu wanapenda kuonekana wamefanikiwa wakati matokeo wanayopata siyo ya mafanikio. Watu wanapenda kuonekana wanajua wakati wanachojua hakiwasaidii kuwa bora. Watu wanapenda kuonekana wana furaha muda wote wakati maisha yao hayaakisi aina hiyo ya furaha. Nilichojifunza kupitia (more…)