Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; KUIBADILI DUNIA NA KUJIBADILI MWENYEWE…

By | August 12, 2018

“Everyone thinks of changing the world, but no one thinks of changing himself.” — Leo Tolstoy Siku mpya, Siku bora na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na (more…)

BIASHARA LEO; Kitu Kimoja Kinachoweza Kuteketeza Biashara Yako Kabisa…

By | August 11, 2018

Watu wamekuwa wanatoa sababu mbalimbali kwa nini biashara zao zimeshindwa. Na unapowasikiliza, utawasikia wakisema mambo ya nje tu. Kwamba uchumi mgumu, kwamba watu hawana fedha, kwamba ushindani umekuwa mkali na mengine kama hayo. Hutawasikia wakisema mambo ya ndani, ambayo ndiyo sababu kuu ya kufa kwa biashara. Mambo kama uzembe, uvivu, (more…)

UKURASA WA 1319; Kwa Nini Njia Za Mkato Zinazidi Kuibuka Kila Siku?

By | August 11, 2018

Moja ya shida ambayo watu ambao hawajafanya maamuzi ya mafanikio wanaipata, ni kuibuka kwa njia za mkato kila siku. Wote tunajua kabisa kwamba hakuna mafanikio yanayopatikana kwa njia ya mkato. Wote tunajua kazi na muda vinahitajika ili mtu aweze kufanikiwa. Wote tunajua safari ya mafanikio inahusisha kushindwa mara nyingi. Lakini (more…)

BIASHARA LEO; Usijiachie Kwa Sababu Biashara Ni Yako…

By | August 10, 2018

Kitu kimoja nakiona kwenye biashara za wengi ni kwamba, wengi hawaheshimu biashara zao. Mtu anapokuwa ameajiriwa ataheshimu sana ajira yake. Atawahi kufika kazini na ataondoka pale muda wa kutoka unapofika. Hatajipangia tu safari zisizohusiana na kazi kama anavyotaka mwenyewe. Na hata jamii itamheshimu, haitamtegemea aamue tu chochote, kwa sababu kila (more…)

UKURASA WA 1318; Vipi Kama Hii Ndiyo Siku Pekee?

By | August 10, 2018

Moja ya vitu vinavyofanya tupoteze muda kwenye maisha yetu, ni wingi wa muda na siku ambazo tunafikiri tunazo. Kila ninapokuwa nafikiria muda, huwa kauli ya Seneca inanijia kwenye akili yangu. Seneca anasema, tatizo la muda siyo kwamba hatuna wa kutosha, bali tunao mwingi kiasi kwamba tunaamua kuupoteza. Hivi unafikiri kwa (more…)

BIASHARA LEO; Njia Bora Ya Kufanikiwa Kwenye Biashara Ni Kuwa Na Ubinafsi Kwako Mwenyewe…

By | August 9, 2018

Kama unataka kuendesha biashara yako vizuri na kama unataka kufanya mambo mazuri kwenye hii dunia, basi jua ya kwamba unahitaji kujijali wewe kwanza kabla ya vitu vingine vyovyote. Ni kweli biashara itakuhitaji uweke juhudi kubwa, itahitaji muda wako mwingi, lakini kama hutajijali wewe mwenyewe kwanza, hutafika mbali. Utaweza kupata matokeo (more…)

UKURASA WA 1317; Njia Rahisi Ya Kuwa Mstoa…

By | August 9, 2018

Ustoa ni falsafa ya matendo, falsafa ya kuishi maisha bora kwenye nyakati ambazo ni ngumu. Ni falsafa ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 2000 na imeweza kuwasaidia wengi, hasa viongozi wa nchi na hata wanajeshi kupambana na nyakati ngumu kwao. Uzuri wa falsafa ya ustoa ni kwamba, huhitaji kubadili chochote (more…)

BIASHARA LEO; Unatumia Mtego Gani Kuwanasa Wateja Wa Biashara Yako?

By | August 8, 2018

Kuwanasa wateja wa biashara yako ni hitaji muhimu sana kwa mafanikio ya biashara. Kwa sababu bila ya wateja kunasa, kuwa na kitu wanachokipata kwako tu, hawawezi kurudi tena kwako. Na kama ambavyo nimekuwa nakuambia, mteja akinunua mara moja kwako, ni hasara kwako. Unaanza kufaidika na mteja pale anaponunua tena na (more…)

UKURASA WA 1316; Zifanye Changamoto Kuwa Nishati Ya Kukuchochea Zaidi…

By | August 8, 2018

Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa siyo ndoto kubwa wanazokuwa nazo, na wala siyo kiwango cha kazi ambacho wapo tayari kuchukua. Bali jinsi ambavyo wanachukulia changamoto. Wanaofanikiwa na wanaoshindwa wote wanakuwa na ndoto kubwa kwenye maisha yao. Na wote wanakuwa tayari kuweka kazi ili kufikia ndoto hizo. Lakini kama wote tunavyojua, hakuna (more…)