Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kujenga Himaya Yako Kibiashara…

By | August 1, 2018

Ili biashara ifanikiwe sana, lazima ijijenge kama himaya, imiliki sehemu kubwa ya soko, iwe na wateja wanaoitegemea biashara hiyo, wanaoiamini na ambao wapo tayari kuwaalika wengine kuja kwenye biashara hiyo. Hivyo badala ya kukazana kupata faida ya muda mfupi kwenye biashara yako, kazana kujenga himaya yako kibiashara, himaya ambayo itakuwa (more…)

UKURASA WA 1309; Pima Ongezeko Na Siyo Pengo…

By | August 1, 2018

Unapoangalia hapo ulipo sasa na kule unakokwenda, kuna nafasi kubwa, kuna pengo kubwa ambalo unapaswa kuliziba ili kufikia yale maisha unayoyataka. Kuna njia mbili za kuangalia nafasi hiyo unayopaswa kuivuka ili kufikia maisha unayoyataka. Njia ya kwanza ni kuangalia pengo ambalo lipo kutoka ulipo sasa mpaka kufika kule unakoelekea. Hii (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UFANISI NI KUSEMA HAPANA…

By | August 1, 2018

People are effective because they say no.” — Peter Drucker Amka mwanamafanikio, Amka kutoka kwenye usingizi usio na mwisho, Amka kutoka kwenye hali ya kutokuchukua hatua, Amka kutoka kwenye hali ya kusubiri uwe tayari, Amka kutoka kwenye kujidanganya kwa kulalamika na kuwalaumu wengine. Kama ipo hatua yoyote unataka kupiga kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Wateja Hawafanani…

By | July 31, 2018

Nimewahi kukuambia usifanye mabadiliko makubwa kwenye biashara yako kwa sababu ya maoni ya mteja mmoja. Maana kumekuwa na tabia ya wafanyabiashara kukata tamaa au kupata hamasa kubwa kwa sababu ya maoni ya mteja mmoja au wachache. Wanakata tamaa pale mteja anapowaambia kwamba wanachouza hakifai au siyo wanachotaka, hivyo wanaona ndiyo (more…)

UKURASA WA 1308; Usikubali Kipaji Chako Kiwe Kikwazo Kwako…

By | July 31, 2018

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu ambao wana vipaji vikubwa kwenye maeneo fulani, huwa hawafanyi vizuri kama wale ambao hawana vipaji. Unakuta kuna watu wana kipaji kikubwa sana, lakini wanaofanya vizuri kwenye maeneo hayo ni wale ambao hawana vipaji. Hii inaonesha kwamba, kwa wengi, kipaji ni kikwazo kwao kufanikiwa, badala ya (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kumjibu Mteja Anayekuambia Wengine Wanauza Kwa Bei Ndogo Kuliko Wewe…

By | July 30, 2018

Kwenye biashara yako, utakutana na wateja wengi wanaotaka uwapunguzie bei. Sasa kama bei zako umepanga kwa usahihi, kwa kuzingatia thamani ambayo wateja wanaipata, hupaswi kupunguza bei. Kwa sababu tabia ya kupunguza bei ina madhara makubwa kwenye biashara yako kwa baadaye, hata kama unaona kwa sasa ina manufaa. Mara kwa mara (more…)

UKURASA WA 1307; Tatizo La Tabia Za Watu Waliofanikiwa…

By | July 30, 2018

Huwa tunasema mafanikio yanaambukizwa. Kwamba kama utafanya kile ambacho waliofanikiwa wanafanya, basi unakuwa na nafasi kubwa ya wewe kufanikiwa pia. Na huu ndiyo umuhimu wa kuzijua tabia za watu waliofanikiwa ili kuweza kuziingiza kwenye maisha yetu pia. Lakini kuna tatizo moja kwenye tabia za watu waliofanikiwa, kadiri unavyozidi kuwafuatilia wengi, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USHINDI MKUU NI KUWA WEWE…

By | July 30, 2018

“To be yourself in a world that is constantly trying to make you something else is the greatest accomplishment.” — Ralph Waldo Emerson Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora (more…)