Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1303; Kama Hujisikii Vizuri, Sababu Ni Huzalishi…

By | July 26, 2018

Kwenye hii dunia, kuna makundi mawili ya watu, Kundi la kwanza ni wazalishaji, hawa ni wale wanaofanya mambo yatokee, wanaozalisha vitu, mawazo au kutoa matokeo fulani ambayo watu wanayatumia kwenye maisha yao. Wazalishaji wanaleta kitu pasipo na kitu, wanaleta uwezekano pasipo na uwezekano, na wanawapa watu wengine kitu cha kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; AMINI KWENYE KILE UNACHOFANYA…

By | July 26, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kuwafanya Wateja Wasikutoroke…

By | July 25, 2018

Kwanza kabisa unapaswa kujua kwamba wateja halisi wa biashara yako wanafanya manunuzi ya kununua kwa hisia na siyo kwa fikra au mantiki. Pia unapaswa kujua kwamba wateja wananunua kwa sababu zao binafsi na siyo kwa sababu wewe unauza. Lakini pia unapaswa kujua, kwamba wateja watanunua kwako, kama wanavutiwa kufanya hivyo, (more…)

BIASHARA LEO; Bobea Kwenye Biashara Unayofanya…

By | July 24, 2018

Huwezi kuwa na majibu ya kila kitu kwenye maisha, lakini unapaswa kuwa na majibu ya kila kitu kwenye biashara yako. Unapaswa kujua kila kitu kinachohusiana na biashara yako, kiasi kwamba unaweza kujibu chochote ambacho mteja anakuuliza. Na hiyo ndiyo kazi yako kama mfanyabiashara, kitu pekee kinachokutofautisha na wachuuzi. Mteja anapofika (more…)

UKURASA WA 1301; Majuto Makubwa Sana Unayotengeneza Kwenye Maisha Yako…

By | July 24, 2018

Kama haupo makini na jinsi unavyoyaendesha maisha yako, utakuwa unajitengenezea majuto makubwa sana kwa baadaye. Majuto ambayo kinapofika kipindi unajutia, unakuwa huna tena la kufanya ili kubadili hali ilivyo kwa wakati huo. Muuguzi Bronnie Warre kwenye kitabu chake cha majuto matano ya watu wanaokufa, kupitia kuwahoji watu waliokuwa wanakaribia kufa, (more…)

BIASHARA LEO; Pima Kila Unachofanya Kwenye Biashara Yako…

By | July 23, 2018

Kuna mambo mengi sana unayoweza kufanya kwenye biashara yako, lakini huwezi kufanya yote, huna muda huo wala nguvu hizo. Hivyo unahitaji kuwa na kipaumbele wa nini ufanye na nini usifanye, kwenye vile utakavyofanya, nini uanze kufanya kabla ya kingine. Kwenye kuchagua kipi ufanye, fanya kile ambacho unaweza kupima kwenye biashara (more…)

UKURASA WA 1300; Dhana Ya Kumaliza Kabisa Changamoto Zote…

By | July 23, 2018

Maisha ni mfululizo wa changamoto, kwamba ukimaliza changamoto moja, unakuwa umekaribisha changamoto nyingine. Dhana ambayo wengi wamekuwa nayo ni kwamba wanaweza kumaliza kabisa changamoto zote ambazo wanazo, kitu ambacho siyo kweli. Ndiyo maana njia yoyote ya mkato unayokutana nayo ya kutatua chochote kinachokukwamisha, haitafanya kazi. Kwa sababu njia ya mkato (more…)