Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

BIASHARA LEO; Usiwapoteze Wateja Wako Kirahisi Hivi…

By | July 22, 2018

Zipo njia nyingi sana za kuwapoteza wateja kwenye biashara yako. Na kwa njia zote, wewe mwenyewe ndiye unayechagua kuwapoteza wateja. Kuna mambo unakuwa umefanya au kutokufanya, ambayo yanachangia wateja kuondoka kwenye biashara yako. Japokuwa njia nyingine ni ngumu kwa upande wako, yaani zikishaanza unaweza usiweze kuzuia kwa haraka, zipo njia (more…)

UKURASA WA 1299; Kamwe Usishushe Kiwango…

By | July 22, 2018

Unapofikiria kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unaanza kwa kujiwekea malengo na mipango mikubwa sana. Unajiwekea malengo makubwa kiasi kwamba watu wa kawaida wakiyasikia wanaona labda umechanganyikiwa, au hujui unachofanya. Lakini kwa kuwa wakati huo unakuwa na hamasa kubwa, huwasikii sana na unajua hakuna linaloshindikana. Ni pale unapoanza kufanya ndiyo (more…)

BIASHARA LEO; Maeneo Sita Unayopaswa Kuwa Sahihi Kwenye Biashara Yako.

By | July 21, 2018

Mafanikio kwenye biashara siyo kitu kigumu kama wengi wanavyofikiri. Ni kujua kanuni sahihi ya mafanikio ya biashara yako, kisha kuifanyia kazi huku ukiwa na subira na uvumilivu. Wengi wanaoshindwa kwenye biashara wanakosa kanuni sahihi ya kufanyia kazi au wanakosa subira na uvumilivu. Na kwa kuwa mafunzo ya biashara ni mengi, (more…)

UKURASA WA 1298; Mabishano Hayajawahi Kuleta Mabadiliko…

By | July 21, 2018

Mabadiliko yanatokea pale mimi na wewe tunapochukua hatua ya kufanya vitu kuwa bora zaidi ya vilivyo sasa. Kwa kuchukua hatua, kufanya kitu, kuweka juhudi zaidi, kuweka muda zaidi, kuweka ubunifu zaidi na kuweka umakini zaidi kwenye chochote tunachofanya. Hakuna mabadiliko ambayo yamewahi kutokana na mabishano, maneno pekee hayabadili chochote, hata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UMEZALIWA KUSHINDA…

By | July 21, 2018

“Men are born to succeed, not fail.” —Henry David Thoreau Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA (more…)

BIASHARA LEO; Jina La Mchezo Ni Mauzo…

By | July 20, 2018

Kitu cha kwanza kitakachofanya biashara istawi au kufa ni mauzo. Hili ndilo eneo linaloleta fedha kwenye biashara na fedha ndiyo damu ya biashara. Kama huuzi huna biashara, kama huuzi biashara itakufa. Mauzo ni eneo muhimu sana kwenye biashara yako, na kama nilivyoeleza kwenye kichwa hapo juu, ndiyo jina la mchezo, (more…)

UKURASA WA 1297; Eneo Pekee La Ushindani Ambalo Hakuna Anayeweza Kukupita…

By | July 20, 2018

Tukisema ukweli kama ulivyo; Kuna watu wana akili kuliko wewe, na huna cha kufanya kuwazidi watu hao akili. Kuna watu wana mtandao mkubwa wa watu wanaojuana nao kuliko wee, na huna cha kufanya kuwazidi watu hao. Kuna watu wanaweza kupewa nafasi nzuri hata kama hawastahili, na huna cha kufanya kwenye (more…)