Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1183; Kanuni Ya Ukuu, Iliyo Rahisi Kuelewa Na Kuishi…

By | March 28, 2018

Watu wanapenda ukuu kwenye maisha, kwenye kazi zao, kwenye taaluma zao, kwenye biashara zao na mengine wanayofanya. Lakini ni wachache ambao wamekuwa wakifikia ukuu kwenye yale wanayofanya. Na kadiri siku zinavyokwenda, kwa zama hizi tunazoishi, ndivyo wachache wanaweza kufikia ukuu. Hii ni kwa sababu, mambo ambayo watu wanafanya, yanapingana kabisa (more…)

UKURASA WA 1182; Fedha Hazina Hisia, Sisi Tunazipa Hisia…

By | March 27, 2018

Fedha ni fedha, ni kipande cha karatasi, au chuma, au tarakimu kwenye kompyuta ambayo imepewa thamani na wote tukakubaliana nayo. Nje ya hapo, fedha haina hisia yoyote ile. Lakini sasa, mtu akiokota, kupewa au kushinda zawadi ya fedha, ataitumia hovyo kuliko fedha ambayo ameitafuta kwa nguvu na jasho! Mtu akiwa (more…)

UKURASA WA 1181; Utapiamlo Wa Akili…

By | March 26, 2018

Tumezoea kusikia utapiamlo wa mwili, ambao huwa unasababishwa na kukosa virutubisho muhimu kwenye chakula, au kupata kwa wingi aina fulani ya virutubisho. Kwa mfano kama mtu atakosa protini kwenye chakula chake, hasa watoto, anapata kwashiakoo, huu ni utapiamlo. Lakini pia kama mtu atakula wanga (sukari) kwa wingi, mwili wake utapata (more…)

UKURASA WA 1180; Kitu Ambacho Dunia Inahitaji Zaidi…

By | March 25, 2018

Moja ya njia ambazo tumekuwa tunatumia kupata mawazo ya biashara au huduma gani tutoe ni kujiuliza dunia inataka nini kisha kuipatia. Kuangalia thamani gani unayoweza kuitoa kwa dunia na watu wakawa tayari kuilipia. Swali hili ni dhahiri na linaleta majibu mazuri sana, lakini majibu yake ni mengi na wakati mwingine (more…)

UKURASA WA 1178; Jinsi Ya Kuacha Tabia Mbaya Kishujaa Na Kikatili…

By | March 23, 2018

Kuna vitu ambavyo watu tumekuwa tunafanya, ambavyo vimeshakuwa tabia kwetu, lakini havitupi matokeo ambayo tumekuwa tunayategemea. Lakini kwa kuwa vitu hivyo vimeshakuwa tabia, inakuwa vigumu kwetu kuacha kuvifanya na kwa kuwa tunaendelea kufanya, tunaendelea kupata matokeo yale yale. Iko hivi rafiki, kipato utakachopata kesho, hakitakuwa tofauti na kile ulichopata jana (more…)